Araqchi akataa takwa la madola ya Ulaya la kurejea Iran katika meza ya mazungumzo
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekataa takwa la madola ya Ulaya la kurejea Iran katika meza ya mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi almemwandikia barua Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na viongozi wengine wa Ulaya kwamba vipi Iran irudi kwenye meza ya mazungumzo ambayo yaliharibiwa na Wamarekani na Wazayuni?
Akihutubu Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na viongozi wengine wa Ulaya wanaoialika Iran kwenye meza ya mazungumzo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, "Wiki iliyopita, tulipokuwa tukizungumza na Marekani, utawala ghasibu wa Israel uliamua kuharibu diplomasia."
Araghchi aliendelea, "Wiki hii, wakati wa mazungumzo yetu na Troika ya Ulaya na Umoja wa Ulaya, Marekani iliamua kuharibu diplomasia. Kwa hiyo, tunaweza kufahamu na kupata natija gani kutokana na hali hii?"
Sayyid Abbas Araqchi ameongeza kuwa, kwa mtazamo wa Uingereza na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, suala la msingi ni kwamba Iran lazima irejee kwenye meza ya mazungumzo. Lakini vipi Iran inaweza kurudi kwa kile ambacho haikuacha, achilia mbali kuharibu?