Baqaei: Iran ina haki ya kustafidi na nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani kwa mujibu wa NPT
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127668-baqaei_iran_ina_haki_ya_kustafidi_na_nishati_ya_nyuklia_kwa_malengo_ya_amani_kwa_mujibu_wa_npt
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa kwa mujibu wa mkabata wa NPT na kifungu cha 4 cha mkataba huo, Iran ina haki kamili ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani, na imeazimia kudumisha haki hiyo kwa hali yoyote ile.
(last modified 2025-06-26T12:25:50+00:00 )
Jun 26, 2025 12:23 UTC
  • Baqaei: Iran ina haki ya kustafidi na nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani kwa mujibu wa NPT

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa kwa mujibu wa mkabata wa NPT na kifungu cha 4 cha mkataba huo, Iran ina haki kamili ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani, na imeazimia kudumisha haki hiyo kwa hali yoyote ile.

Akijibu swali la televisheni ya al Jazeera kwamba Rais Trump anasisitiza kuwa mpango wa nyuklia wa Tehran umeharibiwa kabisa na kwamba "shambulio la Marekani lilikuwa operesheni kamilifu iliyoharibu uwezo wa nyuklia wa Iran, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: “Kilicho muhimu kwangu na ambacho hakipaswa kufichwa kwa maneno upambaji na misimamo mbalimbali ya Marekani ni uhakika kwamba tumeshuhudia pigo mbaya kwa sheria za kimataifa, mamlaka ya NPT na maadili ya jamii ya kimataifa. Jambo muhimu zaidi ni kuwa jamii ya kimataifa inapasa kutambua kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Marekani yalikuwa ni kitendo cha uchokozi dhidi ya ardhi nzima na mamlaka ya kitaifa ya Iran.”

Ismail Baqaei ameongeza kuwa: Ninachopaswa kusema ni kuwa haki ya Iran ya kupata nishati ya nyuklia kwa njia ya amani iko pale pale.

Chini ya NPT na kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha mkataba huo, Iran ina haki kamili ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani, na imeazimia kudumisha haki hii kwa hali yoyote.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aidha amesema kuwa Bunge la Iran limepitisha muswada ambao utasimamisha kikamilifu ushirikiano wa nchi na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), huku Iran ikisisitiza kuwa haitaacha mpango wake wa nyuklia wa kiraia kutokana na mashambulizi makubwa yaliyofanywa na Israel na Marekani.