Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wafanya mazungumzo mjini Makka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128112-mawaziri_wa_mambo_ya_nje_wa_iran_na_saudia_wafanya_mazungumzo_mjini_makka
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia wamekutana na kufanya mazungumzo katika mji mtukufu wa Makka nchini Saudi Arabia.
(last modified 2025-07-09T04:50:36+00:00 )
Jul 09, 2025 04:47 UTC
  • Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wafanya mazungumzo mjini Makka

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia wamekutana na kufanya mazungumzo katika mji mtukufu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Iran na Saudi Arabia ni mataifa mawili yenye nguvu katika eneo la Asia Magharibi, na kustawishwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili kunaweza kudhamini usalama wa kikanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi, amekutana na Faisal bin Farhan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya nchi hiyo mjini Makka.

Mkutano huo umefanyika wakati Araghchi akiwa njiani kurejea nchini kutoka kwenye mkutano wa kilele wa kundi la kiuchumi la BRICS uliofanyika nchini Brazil.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wamejadili na kubadilishana Mawazo kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala ya usalama wa kikanda.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na maudhui ya mazungumzo hayo.

Kabla ya hapo Ismail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kuwa, uhusiano wa pande mbili na hali ya amani na usalama katika eneo zitajadiliwa katika mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Saudia.../