Picha za satalaiti zamsuta Trump; Iran ilikiharibu vibaya sana kituo cha US Qatar
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128202-picha_za_satalaiti_zamsuta_trump_iran_ilikiharibu_vibaya_sana_kituo_cha_us_qatar
Picha mpya za satelaiti zimefichua uharibifu mkubwa uliotokea katika kituo cha anga cha Marekani cha Al Udeid kilichoko nchini Qatar baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Iran mwezi uliopita, na hivyo kusuta madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba kambi hiyo kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi haikudhurika.
(last modified 2025-07-11T14:45:51+00:00 )
Jul 11, 2025 14:44 UTC
  • Picha za satalaiti zamsuta Trump; Iran ilikiharibu vibaya sana kituo cha US Qatar

Picha mpya za satelaiti zimefichua uharibifu mkubwa uliotokea katika kituo cha anga cha Marekani cha Al Udeid kilichoko nchini Qatar baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Iran mwezi uliopita, na hivyo kusuta madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba kambi hiyo kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi haikudhurika.

Picha hizo, zilizochambuliwa na shirika la Habari la Associated Press na kutolewa na taasisi ya Planet Labs PBC, zinaonyesha kuwa kuba la kijiografia linalojulikana kama Radome la vifaa vya ufunguo salama vya mawasiliano vinavyotumiwa na vikosi vya Marekani lilikuwepo kwenye kambi hiyo saa chache kabla ya shambulio la Iran lakini halikuonekana tena kwenye picha zilizofuatia.

Ripoti hiyo imesema, "picha kutoka kwa Maabara ya Sayari zinaonyesha kuba la kijiografia likiwa zima kikamilifu asubuhi ya Juni 23, siku lilipofanyika shambulio la kulipiza kisasi la Iran. Picha zilizofuatia za kuanzia Juni 25 na kuendelea zilionyesha kuba likiwa halipo, likiwa na alama za kuungua zinazoonekana na uharibifu fulani wa jengo lililo karibu."

Hadi kufikia sasa, hakuna jibu rasmi la haraka lililotolewa na mamlaka za Marekani au Qatar kuhusu kiwango cha uharibifu uliosababishwa na shambulio la makombora la Iran dhidi ya kituo cha anga cha Al Udeid.

Baada ya shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran, rais wa Marekani Donald Trump alijaribu kudogosha shambulio hilo na kusema lilikuwa “dhaifu sana".

Japokuwa awali Trump mwenyewe pamoja na mawaziri wake wa ulinzi na wa mambo ya nje walitoa vitisho kwamba endapo Iran itachukua hatua ya kuishambulia kijeshi Marekani itakabiliwa na hujuma kali zaidi, lakini Washington haikuchukua hatua yoyote baada ya shambulio hilo la kulipiza kisasi la Tehran, na badala yake rais wa Marekani akatangaza haraka usitishaji vita wa upande mmoja kwa niaba ya Washington na Tel Aviv, ambao unaendelea hadi sasa.../