Kamanda Mkuu: Jeshi la Iran liko katika hali ya juu ya utayarifu wa kivita
Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iran amethibitisha kwamba Jeshi la Nchi hii linaendelea kudumisha kiwango cha uwezo wake “kamili.” Ametoa kauli hii chini ya mwezi mmoja tangu Majeshi ya Iran yalipojibu haraka na kwa ufanisi mashambulizi ya Israel, yaliyomlazimu adui Muisraeli kuomba kusitisha mapigano.
Kamanda Mkuu wa Makao Makuu ya Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, alitoa kauli hii mjini Tehran Ijumaa katika hafla ya kumbukumbu ya kamanda wa ngazi ya juu wa Kikosi cha Quds cha Hifadhi za Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Afisa huyo alimuenzi shahidi Brigedia Jenerali Mohammad Saeed Izadi , anayejulikana kama Haj Ramezan, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Palestina cha Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye aliuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel.
Akigusia mchango wa shahidi Izadi, Jenerali Mousavi amesisitiza urithi wa kudumu wa kamanda huyo na maafisa wengine wa kijeshi waliokufa shahidi, ikiwa ni pamoja na wale waliouawa katia hujuma ya kichokozi ya Israel mwezi uliopita.
Pia Ijumaa, Meja Jenerali Amir Hatami, kamanda wa Jeshi la Iran, alithibitisha tena dhamira thabiti ya jeshi hilo ya kulinda mipaka yote ya nchi.
Alitaja somo lililojifunza kutokana na vita vya miaka minane vya kulazimishwa vya dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam, dhidi ya Iran, ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ilikabiliana navyo kwa ushujaa na kwa ufanisi bila kupoteza hata chembe moja ya ardhi yake.
Hatami alisema, “Hatuwezi kamwe kuruhusu hata chembe moja ya ardhi ya Iran kutenganishwa,” akiahidi kujitolea kwa jeshi katika kuhifadhi mipaka na uhuru wa taifa.
Kauli hizo za maafisa wakuu wa kijeshi zimejiri baada ya mfululizo wa mashambulizi ya Israel kati ya tarehe 13 hadi 25 Juni dhidi ya maeneo ya kijeshi na kiraia ya Iran, yaliyoilazimu Jamhuri ya Kiislamu kujibu uchokozi wa adui kwa haraka.
Operesheni hiyo ya kulipiza kisasi, iliyopewa jina la “Ahadi ya Kweli III,” ililenga miundombinu muhimu ya kijeshi, kijasusi na viwanda vya Israel. Marekani pia iliingia vitani kwa kushambulia vituo vya nyulia vya Iran.
Baada ya hapo Iran ilitekelelza operesheni ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya uwanja wa ndege wa al-Udeid huko Qatar ambayo ni kambi kubwa zaidi ya jeshi la Marekani katika eneo la Asia Magharibi.
Wakati huo huo Jenerali Mohsen Rezaei kamanda wa zamani wa IRGC, amesema operesheni hizo za kulipiza kisasi zilionyesha uwezo wa Iran wa kupambana kwa wakati mmoja na Marekani na utawala wa Israel. Amesema hakuna nchi yoyote, hata China, ina ujasiri kama wa Iran wa kuhujumu maslahi ya Marekani.