Kamanda wa IRGC: Tupo tayari kuendeleza vita pale vilipoishia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128446
Meja Jenerali Mohammad Pakpour, Kamanda wa Vikosi vya Ardhini vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) ametangaza kwamba majeshi ya Iran yamejipanga kikamilifu kushambulia tena, akiwaonya maadui kwamba uchokozi wowote ujao utakabiliwa na jibu la haraka, na kuendeleza vita hivyo pale vilipoishia.
(last modified 2025-07-19T04:20:45+00:00 )
Jul 17, 2025 14:34 UTC
  • Kamanda wa IRGC: Tupo tayari kuendeleza vita pale vilipoishia

Meja Jenerali Mohammad Pakpour, Kamanda wa Vikosi vya Ardhini vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) ametangaza kwamba majeshi ya Iran yamejipanga kikamilifu kushambulia tena, akiwaonya maadui kwamba uchokozi wowote ujao utakabiliwa na jibu la haraka, na kuendeleza vita hivyo pale vilipoishia.

Kamanda Pakpour ameyasema hayo katika mkutano wa ngazi ya juu na Meja Jenerali Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, uliofanyika mjini Tehran jana Alkhamisi.

Meja Jenerali Pakpour alisisitiza ari ya juu ya vikosi vya IRGC na kusema kuwa vikosi vya jeshi viko katika uratibu kamili na tayari kurudia mashambulizi dhidi ya adui.

Akienzi kumbukumbu za makamanda waliouawa shahidi, Pakpor amesifu misimamo ya kishujaa ya wazalendo wa Iran wakati wa vita vya siku 12 vya hivi majuzi, akiutaja Muqawama wa watu kuwa ni nyenzo kuu ya jeshi.

Kamanda Pakpour ametangaza kwamba kwa uungaji mkono mkubwa wa watu, vita vigumu zaidi na fitna katika historia ya Iran hazikufanikiwa.

"Hatutawaachilia wavamizi. [Ikiwa vita vitaanza tena,] tutaviendeleza kutoka mahali palipokoma," Alionya. Jenerali Hatami, kwa upande wake, pia aliheshimu kumbukumbu ya makamanda wa IRGC waliofariki—hasa Luteni Jenerali Salami—na kusifu urithi wao katika kuimarisha ushirikiano kati ya IRGC na Jeshi.

Amesisitiza kuwa, utawala mbovu wa Israel ni tishio kwa amani na usalama katika eneo na dunia. Umesalia kuwa adui wa Waislamu na utalenga nchi nyingine katika eneo hilo iwapo utapewa nafasi.