Iran yautaka Umoja wa Mataifa kurekodi kukiri Trump kuhusika Marekani katika uvamizi dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i132948-iran_yautaka_umoja_wa_mataifa_kurekodi_kukiri_trump_kuhusika_marekani_katika_uvamizi_dhidi_ya_iran
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameitaka taasisi hiyo ya kimataifa kusajili tamko la Trump la kukiri kuhusika moja kwa moja Marekani katika uchokozi na uvamizi wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Juni mwaka huu.
(last modified 2025-11-16T06:33:27+00:00 )
Nov 08, 2025 10:39 UTC
  • Iran yautaka Umoja wa Mataifa kurekodi kukiri Trump kuhusika Marekani katika uvamizi dhidi ya Iran
    Iran yautaka Umoja wa Mataifa kurekodi kukiri Trump kuhusika Marekani katika uvamizi dhidi ya Iran

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameitaka taasisi hiyo ya kimataifa kusajili tamko la Trump la kukiri kuhusika moja kwa moja Marekani katika uchokozi na uvamizi wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Juni mwaka huu.

Katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, , Saeed Iravani balozi na mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameashiria kukiri Rais wa Marekani kuhusu nafasi ya nchi hiyo katika uvamizi dhidi ya Iran na kubainisha kwamba, "Kukiri huku kuna taathira zisizopingika za kisheria za kimataifa katika kuthibitisha uwajibikaji wa vitendo hivyo vya uchokozi."

Sehemu moja ya barua hiyo inasema: Ningependa kutoa mazingatio kwako Mheshimiwa na wajumbe wa Baraza la Usalama kwa matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani ambapo alikiri kwa uwazi na hadharani kuongoza na kuhusika  Marekani kwa siku kumi na mbili za vitendo vya kichokozi na vita vya jinai vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia tarehe 13 hadi 24 Juni mwaka huu (2025).

Siku ya Alkhamisi, Novemba 6, 2025, Trump aliwaambia waandishi wa habari: "Shambulio la kwanza lilifanywa na Israel [utawala]. Lilikuwa kubwa na lenye nguvu sana [na] mimi binafsi nililiongoza."

Aliongeza: "Wakati [utawala] wa Israel ulipoanzisha mashambulizi ya kwanza dhidi ya Iran, ilikuwa siku kubwa kwa Waisraeli, kwa sababu shambulio hilo lilisababisha uharibifu zaidi kuliko mashambulizi mengine yote."