Larijani: Nchi za Magharibi hazistahili kutoa maoni kuhusu uwezo wa makombora ya Iran
-
Ali Larijani
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema nchi za Magharibi zinatumia uwezo wa makombora wa nchi hii kama njia ya kutekeleza mashinikizo yao na kusisitiza kuwa nchi hizo hazipasi kuzungumzia suala hilo.
Ali Larijani amesema kuwa "mjadala wa sasa kuhusu makombora ya Iran hautokani na wasiwasi wa kiusalama bali unatumika kama chombo cha kushinikiza na kuzuia uwezo wa kiulinzi wa Iran."
Ameongeza kuwa haina maana kwa nchi za Magharibi kutoa maoni kuhusu aina mbalimbali za makombora ya Iran. Larijani ambaye ni msuluhishi wa zamani wa masuala ya nyuklia amesisitiza kuwa nchi za Magharibi pia zinatumia kadhia ya nyuklia kama kisingizio cha uhasama dhidi ya taifa la Iran.
Amesema, Marekani na Ulaya zinaibua masuala kadha wa kadha kuhusu makombora ya Iran ili kuidhibiti Jamhuri ya Kiislamu na kutekeleza hatau zao za kujitanua.
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameendelea kusisitiza kuwa: "Hakuna nchi iliyo na haki ya kuingilia mamlaka ya ulinzi wa taifa la Iran.
Marekani na washirika wake wa Ulaya wamesema mara kadhaa kwamba makubaliano yoyote yatakayofikiwa hapo baadaye kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran lazima yajumuishe miradi yake ya makombora ya balistiki.
Tehran kwa upande wake inapinga suala hilo ikisema kuwa uwezo wake wa kijeshi si suala la kujadiliwa.
Ali Larijani Larijani ameashiria uhusiano wa Iran na Magharibi na msimamo wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu uhuru wa kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi wa nchi hii na kuongeza kuwa: "Iran haina lengo la kuyadhibiti mataifa mengine na wala haitapigi magoti na kuwa chini ya udhibiti wa dola lolote.