Jenerali Hassanzadeh: Mifumo ya ulinzi wa dunia inagwaya mbele ya makombora ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133180-jenerali_hassanzadeh_mifumo_ya_ulinzi_wa_dunia_inagwaya_mbele_ya_makombora_ya_iran
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) mjini Tehran, amezungumzia nguvu zinazozidi kuongezeka za Jamhuri ya Kiislamu za kupambna na madola ya kibeberu duniani na kusema: "Katika vita vya siku 12, mifumo jumuishi ya ulinzi ya kimataifa iligwaya na kuzipigia magoti nguvu za makombora za Iran na adui alihisi kushindwa vitani katika muda usiozidi saa 24.
(last modified 2025-11-15T02:37:00+00:00 )
Nov 15, 2025 02:37 UTC
  • Brigedia Jenerali Hassan Hassanzadeh
    Brigedia Jenerali Hassan Hassanzadeh

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) mjini Tehran, amezungumzia nguvu zinazozidi kuongezeka za Jamhuri ya Kiislamu za kupambna na madola ya kibeberu duniani na kusema: "Katika vita vya siku 12, mifumo jumuishi ya ulinzi ya kimataifa iligwaya na kuzipigia magoti nguvu za makombora za Iran na adui alihisi kushindwa vitani katika muda usiozidi saa 24.

Mwandishi wa Shirika la Habari la Fars ameripoti habari hiyo kutoka Rasht akimnukuu Brigedia Jenerali Hassan Hassanzadeh akisema hayo katika hafla ya kukumbuka ya miaka 10 ya kuuawa shahidi mlinzi wa Haram takatifu, Sayyid Ismail Siratnia na kuongeza kuwa: "Shahidi Siratnia alikuwa muumini wa kweli mwenye ufahamu na mwenye uchungu mkubwa na Mapinduzi ya Kiislamu na mara zote alikuwa mstari wa mbele katika kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu na kutoa huduma kwa familia za mashahidi."

Aidha amesema kwamba shahidi Siratnia alipata hadhi ya juu ya kuuawa shahidi na kuungana na vipenzi na mashahidi wenzake na kuongeza kuwa, kupitia urafiki wake na mashahidi wenzake, shahidi Siratnia aliingia kwenye kila medani ya mapambano kwa uaminifu na ujasiri mkubwa na kwamba Mapinduzi ya Kiislamu yalihitaji mtu kama yeye muda woe na hakushindwa kamwe kutimiza wajibu wake.

Akizungumzia umuhimu wa kumbukumbu za mashahidi, Brigedia Jenerali Hassanzadeh amesema: Maadhimisho na kumbukumbu hizo zinasaidia kushikamana na njia ya mashahidi na kuimarisha utamaduni wa Muqawama na kudumisha amani na utulivu katika jamii sambamba na kuhamasisha kizazi kimpya kuendeleza njia tukufu ya mashahidi.

Vilevile mesema: Adui hajaacha kufanya njama hata sekunde moja kwa nia ya kuyadhuru Mapinduzi ya Kiislamu kwa miaka 47 sasa, lakini ustawi na maendeleo ya mapinduzi haya matakatifu yanaendelea kumkatisha tamaa adui muistikbari.

Akizungumzia matukio ya hivi karibuni katika eneo hili na ushindi wa Muqawama amesema: Ushindi mkubwa zaidi wa taifa la Iran ulipatikana katika Vita vya Siku 12; Wamarekani walikuwa wamepanga kushambulia Iran moja kwa moja kwa zaidi ya miaka saba nyuma, lakini nguvu za Mapinduzi ya Kiislamu zimekuwa zikivunja njama zao muda wote.