Mtaalamu wa Russia: Mkataba wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Iran na Russia; hatua muhimu ya 2025
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135126-mtaalamu_wa_russia_mkataba_wa_ushirikiano_wa_kimkakati_kati_ya_iran_na_russia_hatua_muhimu_ya_2025
Igor Matveev, profesa na mtaalamu wa masuala ya siasa wa nchini Russia ameutaja Mkataba Kamili wa Kimkakati uliosainiwa kati ya Iran na Russia mwanzoni mwa mwaka jana kuwa hatua muhimu katika uhusiano kati ya mataifa haya mawili.
(last modified 2026-01-05T04:15:40+00:00 )
Jan 05, 2026 04:15 UTC
  • Igor Matveev
    Igor Matveev

Igor Matveev, profesa na mtaalamu wa masuala ya siasa wa nchini Russia ameutaja Mkataba Kamili wa Kimkakati uliosainiwa kati ya Iran na Russia mwanzoni mwa mwaka jana kuwa hatua muhimu katika uhusiano kati ya mataifa haya mawili.

Dakta Igor Matveev ni profesa mshiriki katika Idara ya Biashara ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Masuala ya Fedha cha Serikali ya Shirikisho la Russia. 

Dakta Matveev ameangazia masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa, hasa yale yanayozihusu Iran na Russia katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la IRNA  huko Moscow mji mkuu wa Russia. 

Ameutaja Mkataba wa Pamoja wa Kimkakati kati ya Iran na Russia kuwa hatua muhimu na chanya iliyofikiwa mwaka uliopita na kwamba ni ishara ya azma ya nchi mbili ya kusonga mbele kwa ajili ya kufanikisha maslahi yao. 

"Kuna upeo mpana wa kuendeleza ushirikiano wa kimkakati kati ya Shirikisho la Russia na Jamhuri ya Kiislamu," amesema profesa huyo mshiriki katika Idara ya Biashara ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Masuala ya Fedha cha Serikali ya Shirikisho la Russia. 

Ameongeza kuwa: Kujiunga Iran na makundi kama BRICS kunaipa fursa ya kuwa sehemu ya miradi yenye  muhimu kama ule wa ushoroba wa Kaskazini- Kusini.