Anadolu: Iran imeitia Marekani hasara ya dola bilioni 2 hadi sasa, ACP yasema ni dola bilioni 5
-
Kusambaratishwa mfumo wa rada ya tahadhari ya mapema wa AN/FPS 132 wa Marekani
Shirika la Habari la Anadolu limeripoti leo Jumatano kwamba tangu kuanza kwa vita vya sasa vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, Jumamosi iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu imeharibu zana za kivita za Marekani zenye thamani ya dola bilioni mbili.
Hata hivyo kituo cha utafiti wa Juu cha Marekani, CPA, kimekosoa vikali serikali ya nchi hiyo kwa kuanzisha vita vingine Magharibi mwa Asia na kuandika kuwa Donald Trump anatenda kinyume na ahadi zake za uchaguzi.
CPA imefichua kuwa vita dhidi ya Iran vimeisababishia hasara kubwa Marekani na kwamba mbali na kuuawa idadi kadhaa ya wanajeshi wa nchi hiyo, hadi tarehe 3 Machi, yaani katika siku tatu za vita hivyo, Marekani ilikuwa imepata hasara ya dola bilioni 5 za walipakodi wa nchi hiyo.
Shirika la habari la Uturuku, Anadolu limeripoti kuwa, sambamba na tangazo la Jeshi la Ulinzi la Iran la kuendelea kushambulia maslahi ya Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia, vyombo vya habari vya kigeni pia vinaripoti kuwa Marekani imepata hasara kubwa ya zana za kijeshi zinazoendelea kuharibiwa kwa mashambulizi ya Iran.
Ripoti ya shirika hilo inasema tangu kuanza uchokozi dhidi ya Iran, Februari 28, Marekani imepata hasara ya dola bilioni mbili za kuharibiwa zana na taasisi zake za kijeshi.
Baada ya kuchambua data za kijeshi na picha za satalaiti waandishi habari wa Anadolu wameeleza kuwa, hadi sasa Iran imeharibu zana za kijeshi za Marekani zenye thamani ya dola karibu bilioni mbili katika eneo la Asia Magharibi.
Ripoti hiyo imesema, hasara kubwa zaidi iliyosababishwa na mashambulizi ya Iran dhidi ya kambi za Marekani ni mfumo wa rada ya tahadhari ya mapema wa AN/FPS 132 wa Marekani katika kambi ya jeshi la anga ya al Udaida nchini Qatar wenye thamani ya dola bilioni 1.1.