Kamandi ya Khatam al-Anbia: Wanajeshi 100 wa Marekani wameuawa katika shambulizi la Iran huko Dubai
-
Shambulio la Iran huko Dubai
Msemaji wa Kamandi ya Majeshi ya Iran ya “Khatam al-Anbia” ametoa taarifa akisema kuwa wanajeshi 100 wa Marekani wameuawa katika shambulizi la Iran huko Dubai.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Kamandi ya Majeshi ya Iran ya “Khatam al-Anbia” imesema kituo hicho cha mkusanyiko wa wanajeshi magaidi wa Marekani katika mji wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kilikuwa na wanajeshi 160.
Amesema kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia na kutoka uwanjani, wanajeshi 100 wa Marekani wameangamizwa katika shambulizi mseto lililoshirikisha makombora na ndege zisizo na rubani.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa Marekani na washirika wake wanatumia mbinu ya kuficha hasara zinazosababishwa na vipigo mtawala vya mjeshi ya Iran na hata kuwaadhibu wale wanaorusha hewani picha na video za matukio hayo.
Katika muktadha huo, Polisi ya Dubai imetahadharisha kuwa wale wanaochukua picha na video za milipuko ya mashambulizi ya makombora ya Iran kujibu uchokozi wa Marekani watakabiliwa na adhabu ya faini ya karibu dola elfu 60 za Marekani.
Gazeti la Gulf Times limeripoti kuwa, Polisi ya Dubai imewatahadharisha wakazi wa mji huo kwamba ni marufuku kurusha hewani maudhui inayokwenda kinyume na taarifa ya serikali.
Polisi ya Dubai imesema mtu yeyote atakayekiuka tangazo hilo atakabiliwa na adhabu ya kifungo jela na faini ya dirhamu 200,000 (karibu dola 54,400 za Marekani).