Khorramshahr-4 yaingia uwanjani katika operesheni Ahadi ya Kweli 4, yatwanga ngome za Israel
-
Kombora ya Khorramshahr -4
Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) imetangaza kuwa makombora ya Khorramshahr 4, (Khaybar), ya kikosi cha Anga cha jeshi hilo yameanza kutumika kwa kushambulia katikati ya mji wa Tel Aviv, Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion na kambi ya jeshi la anga la Israel katika uwanja huo.
Mashambulizi hayo yameanza kwa jina la msimbo la Yaa Hassan bin Ali (AS).
Taarifa Nambari 21 iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imeeleza kuwa makombora mazito ya Khorramshahr 4 ya kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambayo kichwa cha kila moja ya makombora hayo kina uzito wa tani moja, yamefyatuliwa mapema leo kuelekea Tel Aviv, Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion na kambi ya jeshi la anga la Israel katika uwanja huo katika fremu ya opesheni Ahadi ya Kweli 4.
Mafanikio ya makombora hayo ya kistratijia ya kuvuka salama matabaka saba ya mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel yakitanguliwa na ndege za kivita zisizo na rubani, yamewasababishia Wazayuni Jahanamu halisi.