Msemaji wa IRGC: Silaha mpya za Iran za kukabiliana na uchokozi wa adui Marekani na mzayuni ziko njiani
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC ametangaza kuwa mbinu mpya na silaha mpya ziko njiani kuzinduliwa kwa ajili ya kukabiliana na uchokozi wa kijeshi ulioanzishwa na Marekani na utawala wa kizayuni.
Brigedia Jenerali Ali Mohammad Naeini ameeleza hayo leo Ijumaa na kubainisha kwamba, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimejiandaa kwa vita vya muda mrefu hadi kuhakikisha vimemtia adabu mchokozi.
Jenerali Naeini ameongeza kuwa, katika kila wimbi la operesheni, adui ajiandae kukabiliwa na vipigo vikali.
Msemaji na mkuu huyo wa Idara ya Mawasiliano ya Umma ya IRGC ametangaza pia kwamba, mbinu na silaha mpya za kivita za Iran ziko mbioni kuzinduliwa, na hadi sasa hazijaanza hasa kutumika.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, afisa mmoja wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amenukuliwa akisema kuwa, katika kipindi cha wiki moja iliyopita ya vita Iran imetumia zaidi makombora ya kizazi cha miaka 10 iliyopita katika mashambulizi yake dhidi ya ngome na vituo vya Marekani na utawala wa kizayuni katika eneo…/