Meja Jenerali Abdullahi: Uwezo wa makombora wa Iran ni zaidi ya mawazo ya adui
-
Meja Jenerali Ali Abdullahi
Meja Jenerali Ali Abdullahi, amesema majeshi ya ulinzi ya Iran yamejitayarisha kikamilifu kuendeleza mapambano dhidi ya adui na kwamba adui atapata jibu la makosa yake uwanjani na kwenye medani ya vita.
Meja Jenerali Ali Abdullahi, Kamanda wa Makao Makuu ya Jeshi ya Khatam al-Anbiya (SAW), amesema: "Adui Mmarekani na Mzayuni amekuwa akifanya makosa kila mara, na tumesema mara kwa mara kwamba tutamjibu adui uwanjani; tunatumai kwamba leo wameelewa kwamba sisi si watu wa kutoa kaulimbiu tupu na ni wanaume wa uwanjani."
Meja Jenerali Abdullahi ameongeza: "Silaha zetu ni za kisasa zaidi kuliko hapo awali, zina ustahimilivu wa hali ya juu, usahihi na uwezo mkubwa, na tunatumia uzoefu wa vita vya zamani kuwa uwezo wa uendeshaji wa vita vya sasa; adui sasa anaona athari za nguvu hiyo uwanjani."
Amesema: "Adui amedai mara kwa mara kwamba anazo takwimu za makombora yetu, lakini tunasema yahesabuni kwenye uwanja wa vita ili mjue kwamba hamjui chochote kuhusu uwezo wetu."
Kamanda wa Makao Makuu ya ya Jeshi ya Khatam al-Anbiya (SAW) ameongeza: "Vikosi vyote vya jeshi vipo uwanjani vikiwa na ari na motisha ya juu ya kulipiza kisasi kwa damu ya mashahidi, hasa damu safi ya makamanda na mashahidi wapendwa, na vitaendelea na vita hadi adui atakapojuta."