Wall Street: Kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kunaonyesha kushindwa juhudi za Trump za kuipigisha magoti Iran
-
Ayatullah Mojtaba Khamenei
Vyombo vya habari duniani vimeakisi kwa mapana na marefu kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kama kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Jarida la Uingereza la The Economist limeandika: Wairani hawakuathiriwa na takwa la Trump la kushirikishwa katika kumchagua kiongozi wa baadaye au wito wake wa "kujisalimisha bila masharti."
Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imeripoti kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba umati mkubwa mjini Tehran umeelezea furaha yao kufuatia kuchaguliwa kwa Ayatullah Mojtaba Khamenei kama kiongozi wa tatu wa Mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu.
Gazeti la Russia Today pia limechapisha filamu kutoka mitaa ya Tehran, likiandika kwamba sauti za Allahu Akbar zimesikika sambamba na tangazo la kuchaguliwa Ayatullah Mojtaba Khamenei kama kiongozi mpya wa Iran.
Gazeti la New York Times limeiakisi habari hiyo kwa kichwa cha habari: "Mwana wa Ayatullah Khamenei ndiye kiongozi mpya wa Iran."
Televisheni ya Saudi Arabia ya Al-Hadath imeripoti kuchaguliwa kwa Ayatullah Sayyid Mojtaba Husseini Khamenei kama Kiongozi Mkuu wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuakisi taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kuunga mkono uongozi wake. Imeandika kwamba IRGC na makamanda wa vikosi vya majeshi ya Iran wametangaza utayarifu wao wa kumtii kiongozi mpya.
Shirika la habari la Bloomberg pia limeandika kwamba Iran imemchagua mwana wa Ayatullah Khamenei kama kiongozi wake mpya.
Gazeti la New York Times pia limeandika katika kichwa chake cha habari, "Mwana wa Ayatullah Khamenei ndiye kiongozi mpya wa Iran."
Kwa upande wake, jarida la Wall Street lilisema: Kuchaguliwa Sayyid Mojtaba Khamenei kama kiongozi mpya wa Iran kunaonyesha kushindwa juhudi za Trump za kuipigisha magoti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.