Operesheni Ahadi ya Kweli 4, Wimbi la 33: Makombora yote ya Iran ya “Kheibar Shekan” yapiga malengo yao
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuanza kwa wimbi la thelathini na tatu la Operesheni Ahadi ya Kweli 4, ambapo makombora yote yenye mwongozo wa usahihi ya aina ya “Kheibar Shekan” yalifanikiwa kupiga malengo yaliyokusudiwa.
Kwa mujibu wa ParsToday, wimbi la 33 la Operesheni Ahadi ya Kweli 4 lilitekelezwa kwa kaulimbiu “Labbaik Ya Khamenei” dhidi ya malengo ya adui wa Marekani na Uzayuni.
Katika wimbi hili, idadi kubwa ya makombora ya KheibarShekan yenye mafuta imara na vichwa vya vilipuzi vya uzito wa takribani tani moja yalitumika, na zaidi ya makombora 10 ya KheibarShekan yalipiga Tel Aviv katikati ya maeneo yanayokaliwa.
Kufuatia operesheni hii, kituo cha tano cha kijeshi cha majini cha Marekani kilicho katika ardhi ya Bahrain kililengwa kwa mafanikio.
Baada ya wimbi la thelathini na tatu la Operesheni Ahadi ya Kweli 4, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilitoa taarifa kwa adui likisema: “Hatutaruhusu mpone wala mkimbie.”
Wakati huo huo, katika saa zilizopita, kituo cha kusafisha mafuta na gesi pamoja na matangi ya hifadhi ya mafuta ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Haifa yalishambuliwa na ndege zisizo na rubani (droni) za Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran..
Katika taarifa jeshi limesema mapambano dhidi ya wahalifu wa Marekani na utawala wa Kizayuni unaoua watoto yataendelea hadi ushindi wa mwisho wa kambi ya haki dhidi ya batili.
Vita hivi vya kulazimishwa, vilivyoanza asubuhi ya tarehe 28 Februari kufuatia shambulio la kigaidi la Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, vinaendelea kuwa tata zaidi na vya umwagaji damu kadiri siku zinavyosonga, huku adhabu dhidi ya wavamizi ikiendelea kubaki katika ajenda kuu ya vikosi vya ulinzi vya Iran.