Araqchi: Tel Aviv na Washington zinabeba dhima ya janga la kiuchumi nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137268-araqchi_tel_aviv_na_washington_zinabeba_dhima_ya_janga_la_kiuchumi_nchini_marekani
Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa wanaobeba dhima ya moja kwa moja ya janga la kiuchumi nchini Marekani ni Israel na waungaji mkono wake huko Washington.
(last modified 2026-03-10T10:38:54+00:00 )
Mar 10, 2026 10:38 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa wanaobeba dhima ya moja kwa moja ya janga la kiuchumi nchini Marekani ni Israel na waungaji mkono wake huko Washington.

Sayyid Abbas Araqchi ameandika leo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: Israel na waungaji mkono wake huko Washington wanahusika moja kwa moja na janga la kiuchumi nchini Marekani.

Araqchi ameongeza kuwa: "Iran haitaki kuwadhuru watu wa kawaida wa Marekani, ambao wamepiga kura nyingi kupinga uingilia kati na vita vya kigeni vyenye gharama kubwa."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Israel na vibaraka wake huko Washington wanabeba dhima moja kwa moja na kupanda kwa bei ya petroli, kuongezeka riba ya mikopo ya nyumba na kupungua pakubwa kwa mafao za kustaafu.