Msemaji wa Majeshi ya Iran: US inawatumia watu wa Asia Magharibi kama ngao
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi amesema baadhi ya makamanda na wanajesh wa Marekani wanawatumia raia wa eneo la Asia Magharibi kama ngao za binadamu vitani.
Akijibu bwabwaja na madai mapya ya Trump, Brigedia Jenerali Shekarchi amesema, "Trump, rais mwenye njozi wa utawala mtenda jinai wa Marekani, alianzisha uvamizi wa kikatili dhidi ya taifa letu kwa lengo la kuupa himaya utawala unaoa watoto wa Israel, na kwa kisingizio cha eti kuwalinda wananchi wa Iran."
Amesema baada ya Trump kuona wanajeshi wa Marekani wanakabiliwa na vipigo kutoka Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, aliamua kufidia kushindwa kwake kwa kuwalenga raia wa kawaida hapa nchini.
Jenerali Shekarchi amesisitiza tena dhamira ya vikosi hivyo katika kulilinda taifa na mipaka ya Iran, pamoja na kuimarisha uwezo wake wa mashambulizi.
Msemaji wa Majeshi ya Iran amesisitiza kuwa, taifa kubwa la Iran limevunja kiburi cha Trump, na nguvu hewa za jeshi (la Marekani) ambalo limenasa kwenye kinamasi.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) linaendeleza wimbi la mashambulizi ya Operesheni ya Ahadi ya Kweli 4 dhidi ya kambi na maslahi ya adui Mmarekani na Mzayuni katika eneo la Asia Magharibi.
Vita hivi vya kulazimishwa, vilivyoanza asubuhi ya tarehe 28 Februari kufuatia shambulio la kigaidi la Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, vinaendelea kuwa tata zaidi na vya umwagaji damu kadiri siku zinavyosonga, huku adhabu dhidi ya wavamizi ikiendelea kubaki katika ajenda kuu ya vikosi vya ulinzi vya Iran.
Ikumbwe kuwa, Mnamo Juni 24, Iran, kupitia operesheni za kijeshi zilizokuwa na mafanikio za kujibu uchokozi wa utawala wa Israel na Marekani, ilifanikiwa kulazimisha maadui hao kusitisha uchokozi huo haramu.