Umeme wakatwa kaskazini mwa Tel Aviv kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137576-umeme_wakatwa_kaskazini_mwa_tel_aviv_kufuatia_mashambulizi_ya_makombora_ya_iran
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimeripoti kuwa huduma ya umeme imekatwa katika moja ya miji ya kistratejia ya kaskazini mwa Israel kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran.
(last modified 2026-03-25T07:39:09+00:00 )
Mar 25, 2026 07:39 UTC
  • Umeme wakatwa kaskazini mwa Tel Aviv kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimeripoti kuwa huduma ya umeme imekatwa katika moja ya miji ya kistratejia ya kaskazini mwa Israel kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran.

Shirika la Habari la Iran (IRNA) limeripoti kuwa, vyombo vya habari vya Israel vimetangaza kwamba huduma ya umeme katika mji wa Netanya unaopatikana kaskazini mwa Tel Aviv imekatwa kikamilifu kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran. 

Kuhusiana na suala hili na sambamba na mashambulizi hayo, sauti za ving'ora vya tahadhari ya mapema zimesikika katika mji wa Eilat katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. 

Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) awali ilitangaza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya makombora ya masafa marefu na mafupi na droni zilifanya mashambulizi katika  mji wa Eilat, vituo vya satalaiti vinavyotoa huduma kwa jeshi la Israel linalouawa watoto na kambi za anga za al Azraq, Sheikh Isa, Ali al Salim na Arifjan za jeshi gaidi la Marekani.