Pezeshkian: Taifa la Iran limemfanya adui akate tamaa kwa mapambano yake ya siku 40
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo nafasi muhimu ya Muqawama na mapambano ya kitaifa katika kuvuka kipindi na hali ya vita na kusema: "Taifa la Iran, limemfanya adui akate tamaa na kukosa matumaini kwa Muqawama na mapambano yake ya siku 40."
Akizungumzia utabiri ambao haukuwa sahihi wa maadui kuhusu uwezo wa muqawama na kusimama kidete wa watu wa Iran, Rais Masoud Pezeshkian ameongeza: "Wakati adui akifikiri kwamba Iran haingeweza kupambana kwa zaidi ya siku chache, taifa la Iran, lilimlazimisha kukata tamaa kwa mapambano yake ya siku 40; na hata vitishio vya kuharibu miundombinu havikuweza kuyumbisha azma ya watu wa Iran."
Ameongeza kwa kusema: "Maadui walidhani kwamba kwa kulazimisha vita na mashinikizo, wananchi wangeingia mitaani na kuipindua serikali, lakini watu wenye busara wa Iran wamelinda utawala wa Kiislamu kwa mahudhurio yao makubwa na kuwakatisha tamaa maadui."
Rais Pezeshkian ameutaja mchango muhimu wa ushiriki wa umma, misikiti, na uwezo wa kijamii katika kusimamia migogoro kuwa ndio siri ya ushindi wa Iran, na kusisitiza kwamba: Kutumiwa uwezo huo na mahudhurio athirifu ya wananchi vimekuwa na nafasi muhimu katika kushinda na kuvuka kwa mafanikio hali na mazingira ya hivi karibuni.