Iravani: Silaha zilizotumiwa katika uvamizi dhidi ya Iran zilitoka kwenye maghala ya baadhi ya nchi za Kiarabu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137844-iravani_silaha_zilizotumiwa_katika_uvamizi_dhidi_ya_iran_zilitoka_kwenye_maghala_ya_baadhi_ya_nchi_za_kiarabu
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amepinga madai ya Bahrain, akisema: Mabaki yaliyopatikana kutoka kwenye silaha zilizotumiwa katika mashambulizi ya miji ya Iran yanathibitisha kuwa silaha hizo zilitoka kwenye maghala ya baadhi ya nchi za kiarabu za Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2026-04-16T11:44:07+00:00 )
Apr 15, 2026 08:08 UTC
  •  Amir Saeed Iravani
    Amir Saeed Iravani

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amepinga madai ya Bahrain, akisema: Mabaki yaliyopatikana kutoka kwenye silaha zilizotumiwa katika mashambulizi ya miji ya Iran yanathibitisha kuwa silaha hizo zilitoka kwenye maghala ya baadhi ya nchi za kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Katika barua aliyomwandikia Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja na Rais wa Baraza la Usalama, baada ya madai ya Bahrain kwa niaba ya baadhi ya nchi jirani katika eneo la Ghuba ya Uajemi, Amir Saeed Iravani amefafanua kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga vikali madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na nchi hizo yenye lengo la kupotosha ukweli.

Iravani ameongeza: Kwa mujibu na data za ufuatiliaji na tathmini zilizofanywa na majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wavamizi wametumia mara kwa mara ardhi na anga za nchi hizo kupanga, kuandaa, kuwapa silaha na kutekeleza operesheni haramu za kijeshi dhidi ya Iran.