Iran yatoka sare ya mabao 2 kwa 2 na New Zealand, Misri yagawana pointi na Ubelgiji Kundi G
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139180-iran_yatoka_sare_ya_mabao_2_kwa_2_na_new_zealand_misri_yagawana_pointi_na_ubelgiji_kundi_g
Timu ya Taifa ya Iran, Team Melli, imetoka sare ya mabao mawili kwa mawili na timu ya taifa ya New Zealand katika mechi ya kundi G iliyopigwa uwanja wa SoFi Stadium huko California.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Jun 16, 2026 05:53 UTC
  • Ramin Rezaeian, mchezaji bora wa mechi ya Iran na New Zealand
    Ramin Rezaeian, mchezaji bora wa mechi ya Iran na New Zealand

Timu ya Taifa ya Iran, Team Melli, imetoka sare ya mabao mawili kwa mawili na timu ya taifa ya New Zealand katika mechi ya kundi G iliyopigwa uwanja wa SoFi Stadium huko California.

Ramin Rezaeian, amefunga bao la kwanza la Team Melli na kutengeneza la pili lililowekwa kimiani na Mohammed Mohebi. Kwa New Zealand, mabao yote mawili yamefungwa na Elijah Just, kupitia pasi mbili za Chris Wood.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Ubelgiji imetoka sare ya 1–1 na Misri katika mchezo uliochezwa jioni ya Juni 15,2026

Misri walipata goli la kwanza kupitia Emam Ashour dakika ya 20. Ubelgiji walisawazisha kupitia goli la kujifunga mwenyewe beki wa Misri, katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Kabla ya hapo Uhispania ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa Kundi H.

Matokeo hayo yameifanya kila timu kujikusanyia pointi moja katika msimamo wa kundi hilo, ambalo pia linazijumuisha Saudi Arabia na Uruguay zilizogawana pointi kwa kufungana bao moja kwa moja.

Miamba ya Afrika, Senegal wanaingia dimbani leo kwa ajili ya kunyukana na Ufaransa.. Kila la kheri timu ya Afrika na Iran….