Baqaei: Msaada wa kiufundi na uungaji mkono kwa mvamizi ni sawa na kushiriki katika uvamizi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139490-baqaei_msaada_wa_kiufundi_na_uungaji_mkono_kwa_mvamizi_ni_sawa_na_kushiriki_katika_uvamizi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, utoaji wa huduma za "kiufundi na msaada" kwa pande zinazoshambulia nchi nyingine ni kushiriki moja kwa moja na waziwazi katika kupigana vita haramu vya hiari na ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Jun 28, 2026 09:57 UTC
  • Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, utoaji wa huduma za "kiufundi na msaada" kwa pande zinazoshambulia nchi nyingine ni kushiriki moja kwa moja na waziwazi katika kupigana vita haramu vya hiari na ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Akijibu kauli za maafisa wa Italia waliotaja ushiriki wa nchi hiyo katika vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran kuwa mdogo ulioishia kwenye "msaada wa kiufundi na vifaa" na kwa hivyo wamekana kuwa na ushirikiano wowote katika vita dhidi ya Iran, Ismail Baghaei ameandika kwenye ukurasa wake binafsi:

Huu ni mgongano na hila dhahiri inayolenga kukwepa jukumu la kushiriki katika kosa kubwa la kimataifa: kwa upande mmoja, unakana hadharani kutoa msaada wowote kwa wavamizi, lakini wakati huo huo unasema kwamba ulitoa huduma za "kiufundi na msaada" kwa wahusika wa uvamizi; huduma zilizowezesha vita haramu vya uvamizi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa: "Kutoa huduma za "kiufundi na usaidizi" kwa wahusika wa uchokozi kwa kweli si kitu kingine zaidi ya kuwa kushiriki moja kwa moja na waziwazi katika vita haramu, kitendo cha wazi cha uchokozi na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Hivi karibuni pia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza kwamba, Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) na nchi wanachama wake, zikiwemo Italia na Romania, ambazo Katibu Mkuu wa NATO amekiri waziwazi nafasi yao katika kutekeleza mashambulizi haramu na ya kihalifu dhidi ya Iran, zinapaswa kuwajibishwa kwa aina yoyote ya ushirikiano katika uhalifu uliofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.