Spika wa Bunge la Iran: Wito wa Kiongozi wa "Umoja wa Kitaifa" ni muhimu kwa ushindi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140006-spika_wa_bunge_la_iran_wito_wa_kiongozi_wa_umoja_wa_kitaifa_ni_muhimu_kwa_ushindi
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf amesisitiza kuwa kuzingatia maaagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kuhusu kudumisha umoja wa kitaifa ni muhimu kwa ajili ya ushindi katika mapambano dhidi ya adui.
(last modified 2026-07-19T12:54:47+00:00 )
Jul 19, 2026 12:51 UTC
  • Mohammad Baqer Qalibaf
    Mohammad Baqer Qalibaf

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf amesisitiza kuwa kuzingatia maaagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kuhusu kudumisha umoja wa kitaifa ni muhimu kwa ajili ya ushindi katika mapambano dhidi ya adui.

Qalibaf leo ametuma ujumbe katika akaunti yake katika mtandao wa kijamii wa X uliobainisha kuwa: Kutilia mkazo suala la umoja namshikamano wa kitaifa si pendekezo la kimaadili au kijamii pekee; bali ni sharti muhimu kwa ajili ya ushindi katika mapambano dhidi ya adui."

"Tunapasa kuzingatia na kutilia maanani mwongozo wa kidini na kitaifa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kama sehemu la jukumu letu la kihistoria katika mapambano haya ya kitaifa na katika kuiongoza nchi," ameongeza Spika wa Bunge la Iran.

Mohammad Baqer Qalibaf ameeleza haya siku moja baada ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei kutoa ujumbe wa wito wa umoja wa kitaifa nchini Iran.  

Ujumbe wa Jana wa Ayatullah Mojtaba Khamenei ulieleza kuwa: Kudumisha "umoja wa kitaifa" miongoni mwa wananchi na maafisa katika ngazi zote ni mojawapo ya vipaumbele muhimu zaidi vya nchi.