Droni za Jeshi la Iran zashambulia vituo vya kimkakati vya Marekani nchini Kuwait
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeshambulia vituo vya kimkakati vya jeshi la kigaidi la Marekani katika kambi ya Ahmed al-Jaber huko Kuwait kwa kutumia ndege zisizo na rubani zenye uharibifu mkubwa.
Katika awamu ya 27 ya Operesheni Saeqeh, na kujibu mashambulizi ya hivi karibuni ya jeshi la kigaidi la Marekani dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran hasa shambulio la kikatili dhidi ya makazi ya raia kwenye Kisiwa cha Qeshm, ndege zisizo na rubani za jeshi la Iran zimeshambulia "maegesho ya ndege za kivita", "mifumo ya mawasiliano ya satalaiti" na "maghala ya zana" za jeshi la mauaji ya watoto la Marekani katika kambi ya Ahmad al-Jaber nchini Kuwait.
Kambi ya jeshi ya Ahmed Al-Jaber huko Kuwait imekuwa na nafasi kubwa katika operesheni za anga na usimamizi za Marekani na inatambuliwa kuwa mojawapo ya vituo muhimu vya msaada wa anga kwa jeshi la kigaidi la utawala wa Washington.
Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Iran imelaani shambulio la Marekani dhidi ya nyumba za raia huko Qeshm, ikilitaja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kibinadamu na mfano mwingine wa uhalifu wa kivita wa adui ikisisitiza kuwa: "Uhalifu, vikwazo na vitisho vinaifanya Iran iwe na umoja na imara zaidi katika kujilinda kutakatifu."
Taarifa ya idara hiyo imeongeza: "Mashambulizi makubwa, ya pande zote na mapana ya Jeshi na IRGC yamefelisha juhudii za adui za kuzuia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran, licha ya kutumia mifumo ya ulinzi ya kisasa zaidi, na adui muovu analazimika kuzuia uchapishaji wa habari za uharibifu, vifo na majeraha yanayotokea katika safu zake kupitia udhibiti mkali wa vyombo vya habari."
Mashambulizi ya jeshi la Iran dhidi ya vituo na kambi za kimkakati za Marekani huko Kuwait yanafanyika kulipiza kisasi cha mauaji ya wanafamilia watatu, wakiwemo mama, baba na mtoto wao wa kiume wa miaka miwili, waliuawa shahidi katika shambulio la kinyama la anga la jeshi la kigaidi la Marekani kwenye Kisiwa cha Qeshm kusini mwa Iran.