Vibaraka wawili wa Mossad wanyongwa nchini Iran kwa kutoa taarifa za usalama kwa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140382-vibaraka_wawili_wa_mossad_wanyongwa_nchini_iran_kwa_kutoa_taarifa_za_usalama_kwa_israel
Wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya shirika la ujasusi la Israel, Mossad, wamenyongwa kwa kosa la kutoa taarifa nyeti kuhusu jeshi na maeneo ya usalama ya Iran katika vita vya hivi karibuni vya Marekani na Israel.
(last modified 2026-08-03T09:50:40+00:00 )
Aug 03, 2026 09:48 UTC
  • Iran imenyonga vibaraka wawili wa Mossad.
    Iran imenyonga vibaraka wawili wa Mossad.

Wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya shirika la ujasusi la Israel, Mossad, wamenyongwa kwa kosa la kutoa taarifa nyeti kuhusu jeshi na maeneo ya usalama ya Iran katika vita vya hivi karibuni vya Marekani na Israel.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo Jumatatu, Mahakama ya Iran imesema watu walionyongwa, waliotambuliwa kwa majina ya Omid Behzad na Pouria Safvat, walikuwa "mamluki" wa utawala wa Israel na "wasaliti" wa nchi yao.

Imeongeza kuwa wawili hao walitoa viwianishi, picha na taarifa za kijasusi zinazohusiana na vituo vya kijeshi na usalama vya Iran kwa maafisa wa Mossad na mitandao ya mawasiliano zilizounganishwa na huduma ya ujasusi ya Israel wakati wa vita vya siku 12 mnamo Juni 2025 na uchokozi wa siku 40 wa mwezi Februari mwaka huu na kuwasaidia kutimiza malengo yao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mossad ilijaribu kukusanya taarifa zinazohitajika kutoka ndani ya Iran kabla na wakati wa mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani na Israel kwa kuajiri mawakala wa ndani kupitia mtandao wa njia za mawasiliano za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Imesema kuwa baadhi ya vibaraka hao waliendeleza mawasiliano ya moja kwa moja na maafisa wa ujasusi wa Mossad huku wengine wakituma taarifa zilizohitajika kwa adui kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vinavyohusiana na Israel.

Mahakama ya Iran imeeleza zaidi kwamba vibaraka hao wawili walikuwa washirika wa ngazi ya uwanjani na mawakala wa uendeshaji wa adui na walishiriki katika miradi inayoonekana kuwa rahisi lakini tata sana ya kukusanya taarifa za kijasusi, wakiwa na nafasi muhimu katika kutuma taarifa muhimu kwa maadui wa Iran.

Taarifa hiyo imesema, mashirika ya ujasusi ya Iran yalitekeleza "mojawapo ya miradi muhimu zaidi ya utambuzi" baada ya kufuatilia shughuli za vituo vya habari na vikundi vilivyounganishwa na Israel na kuchambua video zilizotumwa kutoka maeneo ambayo baadaye yalishambuliwa na adui.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa maafisa wa Shirika la Ujasusi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) walifanikiwa kuwatambua na kuwakamata Behzad na Safvat walipokuwa wakishirikiana na maafisa wa ujasusi na Israel.