Waziri wa Afya wa Iran alaani shambulio la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo wa Lamerd Februari mwaka huu
-
Uwanja wa michezo wa Lamerd nchini Iran ulioshambuliwa na Marekani
Waziri wa Afya wa Iran kwa mara nyingine tena amelaani shambulio lililofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo katika mji wa Lamerd mwanzoni mwa mashambulizi ya nchii hiyo na utawala katili wa Israel mwezi Februari mwaka huu hapa nchini lililosababisha vifo kuwajeruhi raia kadhaa.
Mohammad-Reza Zafarqandi ameitaja hujuma hiyo ya Marekani kuwa janga la binadamu wakati alipotembelea eneo hilo ili kutathmini hatua na mahitaji ya huduma za afya zinazohitajika.
Waziri wa Afya wa Iran amesema kuwa ziara yake ililenga kukagua miundombinu ya huduma za afya katika eneo hilo, kutathmini utendaji wa mifumo ya tiba na afya wakati wa hali ya dharura, na kufuatilia mahitaji ya eneo hilo katika uga wa matibabu na huduma za dharura.
Zafarqandi amelaani vikali shambulio la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo wa Lamerd, ambalo liliuwa shahidi na kujeruhi raia kadhaa wa Iran kuanzia mtoto wa miaka miwili hadi vijana na kuutaja uchokozi huo kuwa ni jinai ya wazi dhidi ya watu wasio na ulinzi.
Katika ziara hiyo huko Lamerd, Waziri wa Afya wa Iran pia amekagua hospitali na kuzungumza na madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine wa afya waliotoa huduma baada ya hujuma ya Marekani mapema mwaka huu, na kuwashukuru kwa juhudi zao za kuwapokea, kuwatibu na kuwahudumia watu waliojeruhiwa katika shambulio hilo.
Amesema, Wizara ya Afya inaunga mkono kupanua huduma za matibabu huko Lamerd, akiahidi kuwa hatua zitachukuliwa ili kuimarisha nguvukazi ya hospitali hiyo, kutoa vifaa muhimu na kushughulikia mapungufu yaliyopo.
Amin Niakan Naibu Mkuu wa Masuala ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Shiraz pia amewasilisha ripoti wakati wa ziara hiyo kuhusu utaratibu wa kukabiliana na dharura, mpangilio wa huduma za matibabu na namna majeruhi wa shambulio la Marekani walivyohudumiwa.
Mnamo tarehe 28 Februari, siku ambayo Marekani na Israel zilianzisha vita dhidi ya Iran, Washington iliushambulia uwanja mkubwa wa michezo katika mji wa Lamerd, huko kusini mwa Iran kwa kutumia kombora linalolenga kwa usahihi wa hali ya juu la (PrSM), na kuua shahidi vijana 21 waliokuwemo ndani ya uwanja huo.
Marekani siku hiyo hiyo iliishambulia pia Shule ya Msingi ya Shajarehe Tayyebeh huko Minab kusini mwa Iran kwa makombora ya Tomahawk na kuuwa wanafunzi na walimu wasiopungua 175.