Araqchi: Mazungumzo na Oman kuhusu Lango-Bahari la Hormuz yako katika hatua za mwisho
-
Sayyid Abbas Araqchi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema leo kwamba mazungumzo na Oman kuhusu Lango Bahari la Hormuz yako katika hatua za mwisho na kuongeza: "Bila shaka, hii haina maana kwamba Lango la Hormuz litafunguliwa. Ufunguzi wa Lango la Hormuz unategemea masharti mengine."
Akizungumza leo Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje Sayyid Abbas Araqchi ametangaza kuwa mazungumzo ya Iran na Oman kuhusu Lango-Bahari la Hormuz yamepiga hatua, akisema: "Mazungumzo na Oman yanahusu kuainisha njia mpya ya baharini kupitia Lango-Bahari la Hormuz. Mazungumzo haya yanaendelea vizuri na yako katika hatua za mwisho."
Ameongeza kuwa: "Njia za zamani zitabadilishwa, na nafasi yake inachulikuwa na njia mpya. Wataalamu wanafanya kazi kwenye ramani."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekumbusha kuwa: "Bila shaka, hii haimaanishi kufunguliwa Lango-Bahari la Hormuz. Makubaliano yanaweza kufikiwa, lakini kufunguliwa lango-bahari kunategemea kutimizwa masharti mengine ambayo yametolewa na wapatanishi."
Sayyid Abbas Araqchi ameendelea kuwaambia waandishi wa habari kwamba: "Njia za baharini za Lango-Bahari la Hormuz ziliainishwa mwaka 1968. Wakati wa vita vya hivi karibuni, ilionekana kwamba njia hizi lazima zibadilishwe na kwamba ni muhimu kufanya mabadiliko kwenye njia za baharini, jambo ambalo wataalamu wetu wanafanya kwa sasa na Waomani."
Araghchi pia amesema: Kwa sasa hatuna mazungumzo yoyote na Marekani.
Amesema: "Kuna ubadilishanaji wa ujumbe kupitia wapatanishi. Hii haiitwi mazungumzo, inaitwa ubadilishanaji wa ujumbe. Wapatanishi bado wanajaribu kutengeneza misingi ya mazungumzo."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefafanua kwa kusema: "Kwa maoni yetu, hakuna uwezekano wa kuanza tena mazungumzo hadi pale ukiukwaji wa mkataba wa maelewano utakapokoma na Marekani ifidie kile ilichokiuka katika mkataba huo wa Islamabad.