Qalibaf awapongeza makamanda wa ngazi ya juu kwa uteuzi wao katika majeshi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140592-qalibaf_awapongeza_makamanda_wa_ngazi_ya_juu_kwa_uteuzi_wao_katika_majeshi_ya_iran
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amewapongeza makamanda na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa jeshi walioteuliwa kushika nyadhifa muhimu za kijeshi.
(last modified 2026-08-11T11:29:17+00:00 )
Aug 11, 2026 11:27 UTC
  • Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf
    Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amewapongeza makamanda na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa jeshi walioteuliwa kushika nyadhifa muhimu za kijeshi.

Katika ujumbe wake, Qalibaf amempongeza Meja Jenerali Ali Abdollahi kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Iran na kusifu nafasi mchango wa Abdollahi katika mashambulizi ya karibuni ya Marekani na Israel, na kusema utendaji wake ulidhihirisha nguvu ya vikosi vya ulinzi vya Iran.

"Ninakupongeza kwa dhati kwa uteuzi wako unaostahiki uliofanywa na Amiri Jeshi Mkuu, wa kuongoza Makao Makuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," ameleza Qalibaf.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ametaja wadhifa wa Mkuu wa Majeshi kuwa ni "jukumu kubwa na la kistratejia" na kueleza kuwa Jenerali Abdollahi atafuata nyayo za makamanda waliomtangulia wakiwemo shahidi Meja Jenerali Mohammad Bagheri na Shahidi Meja Jenerali Amir Ali Hajizadeh, ambao walisabilia maisha yao kulinda uhuru na maslahi ya taifa la Iran.

Qalibaf pia alimpongeza Meja Jenerali Ahmad Vahidi kwa kuteuliwa kuwa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

"IRGC imethibitisha kuwa ni nguzo imara na ya kutegemewa kwa wananchi watukufu wa Iran. Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu liliwajibika kama nguzo ya kutegemewa kwa ajili ya kulinda mamlaka ya kujitawala na kuunga mkono nguvu ya taifa chini ya uongozi wa Jenerali Vahidi katika vita vya hivi karibuni," ameongeza kusema Spika kwa Bunge la Iran. 

Mohammad Baqer Qalibaf amepongeza pia Brigedia Jenerali Kiumars Heydari aliyeteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Majeshi ya Iran na kuwapongeza pia makamanda wengine walioteuliwa jana na Ayatullah Sayyid Mojtabda Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kushika nyadhifa za juu za kijeshi.