Tehran: Taarifa ya Ufaransa na washirika wake wa Magharibi dhidi ya Iran ni propaganda za kinafiki za kupotosha ukweli
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140666-tehran_taarifa_ya_ufaransa_na_washirika_wake_wa_magharibi_dhidi_ya_iran_ni_propaganda_za_kinafiki_za_kupotosha_ukweli
Kaimu Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hatua ya Ufaransa na baadhi ya nchi za Magharibi ya kutoa taarifa ya pamoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kisingizio cha masuala ya haki za binadamu na kusema kuwa hatua hiyo ni mfano wa wazi wa unafiki wa kupotosha uukweli wa mambo.
(last modified 2026-08-14T10:11:22+00:00 )
Aug 14, 2026 10:09 UTC
  • Iran yalaani taarifa ya Ufaransa na washirika wake dhidi ya Tehran
    Iran yalaani taarifa ya Ufaransa na washirika wake dhidi ya Tehran

Kaimu Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hatua ya Ufaransa na baadhi ya nchi za Magharibi ya kutoa taarifa ya pamoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kisingizio cha masuala ya haki za binadamu na kusema kuwa hatua hiyo ni mfano wa wazi wa unafiki wa kupotosha uukweli wa mambo.

Hamid Ahmadi, Kaimu Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesema, hatua ya Ufaransa na baadhi ya nchi za Magharibi ya kutoa taarifa ya pamoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kisingizio cha masuala ya haki za binadamu ni hatua ya kujirudia inayolenga kukwepa kuwajibishwa nchi hizo kutokana na ukiukaji wao mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu katika maeneo mbalimbali duniani, yakiwemo Afrika na eneo la Asia Magharibi, hususan kuhusiana na raia wa Iran.

Ahmadi akikumbusha historia chafu ya ukoloni wa Ufaransa barani Afrika na katika maeneo mengine ya dunia, pamoja na hatua uingiliaji wa nchi hiyo katika baadhi ya mataifa ya Afrika ambazo, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, zimesababisha mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya mamilioni ya watu wasio na hatia, aliwashauri viongozi wa Ufaransa kwamba badala ya kuwahubiria wengine, wanapaswa kurekebisha mienendo yao ya kibaguzi dhidi ya raia wa nchi nyingine na wahamiaji, na kusitisha uungaji mkono wao wa kila hali, usio na masharti na usio wa kibinadamu kwa utawala wa Kizayuni unaofanya mauaji ya kimbari na unaokalia kwa mabavu maeneo ya watu wengine.

Kabla ya hapo pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, aalikuwa ameilaani vikali Ufaransa na mataifa mengine kwa kujifanya mawakili wa haki za binadamu na sheria za kimataifa, wakati wakihalalisha na kuunga mkono uhalifu wa kivita unaofanywa na tawala za kigaidi za Israel na Marekani.