Qalibaf: Nilisitisha mazungumzo baada ya shambulio la Israel dhidi ya Dahiyeh huko Beirut
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140694-qalibaf_nilisitisha_mazungumzo_baada_ya_shambulio_la_israel_dhidi_ya_dahiyeh_huko_beirut
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa alisitisha mazungumzo kufuatia shambulio la Israel dhidi ya eneo la Dahiyeh mjini Beirut nchini Lebanon, na kusema kuwa Iran itaushambulia utawala huo haraka iwezekanavyo.
(last modified 2026-08-16T03:07:40+00:00 )
Aug 16, 2026 03:05 UTC
  • Mohammad Baqer Qalibaf
    Mohammad Baqer Qalibaf

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa alisitisha mazungumzo kufuatia shambulio la Israel dhidi ya eneo la Dahiyeh mjini Beirut nchini Lebanon, na kusema kuwa Iran itaushambulia utawala huo haraka iwezekanavyo.

Akizungumza jana katika mkutano na shakhsia watajika katika uga wa utamaduni Mohammad Baqer Qalibaf amesema: "Katika shambulio la hivi karibuni dhidi ya Dahiyeh, nilisitisha mazungumzo na kutangaza kwamba: 'Usiku huu, tutaushambulia utawala wa Israel, na iwapo utawala huo utajibu mapigo, tutashambulia eneo zima. Amesema matokeo yake ni kwamba " mzingiro uliondolewa usiku huo."

Afisa huyo mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran pia ameashiria mazungumzo kuhusu Lango la Hormuz na kueleza kuwa: Kufunguliwa tena njia hiyo kulikuwa kumepangwa kufanyika ndani ya siku 30 kwa mujibu wa makubaliano.

Ameongeza kuwa, baada ya Rais Donald Trump wa Marekani alisema katika mtandao wa kijamii kwamba mzingiro na Lango Bahari la Hormuz vitafunguliwa kwa pamoja usiku, alionya, "Ikiwa madai ya uwongo kuhusu Lango la Hormuz hayatarekebishwa, tutafanya shambulio."

Kwa mujibu wa Qalibaf, Trump alilazimika kurekebisha kauli yake hiyo.

Spika wa Bunge la Iran ameeleza kuwa Kambi ya Muqawama na Lebanon vilijumuishwa katika kipengele cha kwanza cha Hati ya Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran na Marekani.

Mnamo Julai 17, Iran na Marekani zilisaini Mkataba wa maelewano (MoU) wenye vipengele 14 unayosimamiwa na Pakistan, ambao ulitaka kukomeshwa uhasama wa kudumu katika pande zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon, pamoja na kuondolewa mzingiro wa majini dhidi ya Iran ndani ya siku 30, na kurejeshwa usafiri wa kibiashara kupitia Lango-Bahari la Hormuz.