Meja Jenerali Hatami: Ni muhali kwa vituo vya kijeshi vya Marekani kurejea katika hali ya awali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140744-meja_jenerali_hatami_ni_muhali_kwa_vituo_vya_kijeshi_vya_marekani_kurejea_katika_hali_ya_awali
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami amesema Marekani haina tena ruhusa wala haki ya kuingia katika Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman na Mlango Bahari wa Hormuz, akisisitiza kuwa vituo vya kijeshi vya Marekani katu haviwezi kurejea katika hali iliyokuwepo awali.
(last modified 2026-08-17T12:04:12+00:00 )
Aug 17, 2026 12:02 UTC
  • Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami
    Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami amesema Marekani haina tena ruhusa wala haki ya kuingia katika Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman na Mlango Bahari wa Hormuz, akisisitiza kuwa vituo vya kijeshi vya Marekani katu haviwezi kurejea katika hali iliyokuwepo awali.

Meja Jeneralii Hatami amesema hayo katika hafla ya kuwapongeza wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari, huku akipinga madai ya Rais wa Marekani kuhusu Mlango wa Hormuz na kuondoka kwa vikosi vya Marekani katika maji ya eneo hilo.

Kamanda huyo amesema juhudi za Marekani za kuugeuza Mlango Bahari wa Hormuz kuwa “eneo la jinai” hazitafanikiwa. Amesema Iran ina walinzi ambao hawataruhusu mvamizi yeyote kuvamia eneo lake, na kwamba hata madai yatakapotolewa kwa mzaha, yatakabiliwa na jibu kali.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Meja Jenerali Hatami amesema Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetenga zawadi ya dola 30,000 kwa mtu yeyote atakayefanikiwa kumuua au kumkamata na kumkabidhi mwanajeshi wa Marekani anayevamia Iran.

Hatami pia amesema, wanawake wa Iran watakaofanikiwa kufanya hatua hiyo watapewa zawadi mara mbili ya kiasi kinachotolewa kwa wengine. Aidha, amesema silaha zilizotumika katika operesheni hizo zitanunuliwa tena kwa bei mara mbili ya thamani yake na kubadilishwa kwa silaha mpya.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amehitimisha kwa kuutaja Mlango wa Hormuz kuwa “rasilimali ya kijiografia iliyotolewa na Mwenyezi Mungu” na mojawapo ya nyenzo muhimu zaidi za Iran katika kukomesha mivutano na vita.

Amesema kwa kujiamini kuwa, Jeshi la Iran litalinda kikamilifu Mlango huo kwa kufuata maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi, akisisitiza kuwa usimamizi wa nyenzo hiyo ya kimkakati ni mojawapo ya masharti muhimu ya kuondoa tishio la vita dhidi ya wananchi wa Iran.