Iran yamtahadharisha Trump kuhusu 'fikra potofu' ya kudai Mlango-Bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140784-iran_yamtahadharisha_trump_kuhusu_'fikra_potofu'_ya_kudai_mlango_bahari_wa_hormuz_ni_eneo_la_marekani
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa Marekani kwa madai yake kuhusu Lango la Bahari la Hormuz, akionya kuwa "fikra yake potofu" ya kuihesabu njia hiyo muhimu ya maji kama "eneo jipya la Marekani" inapasa kurekebishwa, la sivyo Tehran itamweka sawa.
(last modified 2026-08-19T04:17:53+00:00 )
Aug 19, 2026 04:16 UTC
  • Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi
    Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa Marekani kwa madai yake kuhusu Lango la Bahari la Hormuz, akionya kuwa "fikra yake potofu" ya kuihesabu njia hiyo muhimu ya maji kama "eneo jipya la Marekani" inapasa kurekebishwa, la sivyo Tehran itamweka sawa.

"Kama vile Trump alivyoiitaja Ghuba ya Uajemi kwa jina lake sahihi; fikra yake potofu kuhusu Lango la Hormuz hivi karibuni imma itaondolewa, au tutamweka sawa mtu huyo mwenye mawazo potofu," Gharibabadi ameandika kwenye X akimtahadharisha Rais wa Marekani.

Rais wa Marekani bila kutoa maelezo jana Jumanne alichapisha picha kwenye jukwaa lake la Truth Social inayoonyesha ramani iliyolitaja Lango la Hormuz kama "Eneo Jipya la Marekani,".

Chapisho hilo limeshuhudiwa siku chache baada ya Trump kudai kuwa "hivi karibuni" angetangaza njia ya maji ya Ghuba ya Uajemi kuwa eneo la Marekani.

Pia alitishia kuishambulia Oman iwapo itaingilia kati juhudi zake za kufikia makubaliano na Iran kuhusu Lango la Hormuz.

"Oman ikiingilia kati tutawashambulia na kuwasambaratisha kikamilifu," Trump alisema siku ya Jumatatu.

Trump ameitishia Oman, mshirika wa Marekani baada ya kukabiliwa na hali ngumu sasa kufuatia kushindwa kuhitimisha vita alivyovianzisha dhidi ya Iran na kufikia makubaliano kuhusu Lango la Hormuz.

Awali, Iran ilikubali kuacha Mlango-Bahari wa Hormuz wazi kwa usafirishaji wa kibiashara kwa muda wa siku 60 kufuatia kutiwa saini kwa hati ya makubaliano (MoU) na Marekani mnamo tarehe 17 Juni.

Baada ya Marekani kukiuka masharti ya makubaliano hayo, ikiwemo ahadi yake ya kusitisha mashambulizi katika nyanja zote baadaye Tehran ilikataa kurejea kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Washington.

Badala yake, Iran ilianza mazungumzo na Oman kuhusu hatima ya njia hiyo ya maji, huku ikiainisha masharti mapya ili kurudi kwenye mazungumzo yoyote na Washington. Masharti hayo ni pamoja na kuondolewa kwa vikwazo visivyo halali, kuachiliwa mali za Iran zilizozuiliwa, na kukomeshwa kikamilifu uchokozi wa Marekani.