Jenerali Shekarchi: Zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Israel waliuawa katika vita na Iran
-
Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, Msemaji mkuu wa vikosi vya majeshi ya Iran
Msemaji mkuu wa vikosi vya majeshi ya Iran amesema: "Zaidi ya wanajeshi elfu moja wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuawa katika vita na Iran na maelfu yaw engine wamejeruhiwa."
Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, amesema: "Jeshi la Marekani ni jeshi la Hollywood na propaganda ambalo liliundwa ili kupora na kuiba rasilimali za nchi za Kiislamu; heshima yetu kubwa ni kwamba tumefichua sura ya Kihollywood ya jeshi la Marekani na utawala wa Kizayuni, na ulimwengu mzima umegundua jinsi majeshi haya mawili yalivyo dhaifu na yasiyo na ushujaa."
Ameongeza kuwa: Leo hii nchi za dunia na hata baadhi ya nchi ambazo zina kambi za kijeshi za Marekani, haziwaamini tena Wamarekani, na zimefikia hitimisho kwamba, Marekani ambayo haiwezi kujilinda inawezaje kuwalinda na kuwatetea washirika wake.
Kuhusu wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita vyake dhidi ya Iran, Jenerali Shekarchi amesema: "Kwa mujibu wa ushahidi na vielelezo vya kimazingira, Marekani imepoteza mamia ya wanajeshi katika vita vya tatu vilivyoanzishwa dhidi ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na maelfu ya wanajeshi wa Marekani wamejeruhiwa katika vita hivyo.
Ameongeza kuwa katika uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Iran, kwa ushirikiano wa jeshi la Marekani, zaidi ya wanajeshi elfu moja wa utawala wa Kizayuni wameuawa na maelfu ya wamejeruhiwa.
"Wamarekani na utawala wa Kizayuni wanasema uongo na kuficha ukweli katika kutangaza idadi ya wanajeshi wao waliouawa. Kwa mfano, hutoa takwimu za wanajeshi waliouawa katika vita vya Afghanistan na Iraq miaka kadhaa baada ya mwanajeshi wa Marekani kuuawa, na kisha hukabidhi mwili wake kwa familia yake," amesema Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi.