Kiongozi Muadhamu awasamehe na kuwapunguzia vifungo wafungwa zaidi ya 2,500 kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume SAW
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141118-kiongozi_muadhamu_awasamehe_na_kuwapunguzia_vifungo_wafungwa_zaidi_ya_2_500_kwa_mnasaba_wa_maadhimisho_ya_kuzaliwa_mtume_saw
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ameidhinisha kusamehewa kikamilifu au sehemu ya adhabu wafungwa zaidi ya 2,500 kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume SAW.
(last modified 2026-09-03T12:21:49+00:00 )
Sep 01, 2026 03:30 UTC
  • Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei
    Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ameidhinisha kusamehewa kikamilifu au sehemu ya adhabu wafungwa zaidi ya 2,500 kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume SAW.

Kwa mnasaba wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W.), amri imetolewa ya kusamehe, kupunguza au kubadilisha adhabu kwa wafungwa 2,577 waliotiwa hatiani na mahakama za kawaida na za Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na waliohukumiwa na Mahakama ya Kijeshi na Taasisi ya Adhabu za Serikali la Iran.

Sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad al-Mustafa (S.A.W.) na Imam Jaafar Sadiq (A.S.), Hujjatul-Islam na Muslimin Gholam-Hossein Mohseni Ejei, Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, alimtumia barua Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akiomba kusamehewa, kupunguziwa au kubadilishiwa adhabu kwa watu 2,577 waliotiwa hatiani na Mahakama za Kawaida na za Mapinduzi ya Kiislamu, Shirika la Mahakama za Vikosi vya Jeshi, pamoja na Taasisi ya Adhabu za Serikali la Iran.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amekubali ombi hilo na kumkabidhi Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran jukumu la kufanya uamuzi kuhusu suala hilo.

Hujjatul-Islam na Muslimin Ejei, baada ya kufanya uchunguzi na tathmini zinazohitajika, pia alitoa amri ya kutekelezwa kwa msamaha, kupunguzwa au kubadilishwa kwa adhabu za watu hao waliotiwa hatiani.