Mbunge wa Iran ahoji namna Marekani inavyoshindwa kutofautisha shabaha za kijeshi na maeneo ya raia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141152-mbunge_wa_iran_ahoji_namna_marekani_inavyoshindwa_kutofautisha_shabaha_za_kijeshi_na_maeneo_ya_raia
Hasan Ghashghavi, msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amehoji namna Marekani inavyoshindwa kutofautisha kati ya shabaha za kijeshi na maeneo ya raia kufuatia shambulio la majeshi ya nchi hiyo dhidi ya sherehe ya harusi huko Sirik, katika Mkoa wa Hormuzgan nchini Iran.
(last modified 2026-09-02T12:55:23+00:00 )
Sep 02, 2026 12:53 UTC
  • Hasan Ghashghavi
    Hasan Ghashghavi

Hasan Ghashghavi, msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amehoji namna Marekani inavyoshindwa kutofautisha kati ya shabaha za kijeshi na maeneo ya raia kufuatia shambulio la majeshi ya nchi hiyo dhidi ya sherehe ya harusi huko Sirik, katika Mkoa wa Hormuzgan nchini Iran.

Ghashghavi ametoa kauli hiyo katika chapisho alilotuma kwenye mtandao wa X leo Jumatano, akikosoa shambulio la Marekani lililoilenga sherehe ya harusi katika mji wa pwani wa Sirik, jana usiku.

“Utawala unaodai kuwa mfumo wake wa satalaiti unauwezesha kufuatilia kwa karibu mienendo ya hata kiumbe mdogo zaidi duniani, unawezaje kushindwa kutofautisha kati ya shabaha za kijeshi na shule au sherehe ya harusi?,” ameandika msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Bunge la Iran.

Ameongeza kuwa Marekani na washirika wake wamekuwa wakidondosha mabomu na kurusha makombora dhidi ya watu wasio na hatia kwa miongo kadhaa sasa, huku wakiliachia jukumu la kuhalalisha uhalifu wao kwa kamati za uchunguzi.

Mashambulio ya Marekani dhidi ya maeneo mbalimbali katika ya Mkoa wa Hormuzgan usiku wa Jumanne yalilenga maeneo ya Bandar Abbas, Sirik, Jask, na Qeshm. Eneo la makazi ya raia na sherehe ya harusi katika Wilaya ya Sirik ni miongoni mwa maeneo yaliyolengwa katika mashambulio hayo. Watu wasiopungua watano wameuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika hujuma hiyo ya Marekani.

Iran imejibu kwa mashambulizi makubwa na mapana yaliyolenga kambi na vituo vya kijeshi vya Marekani katika nchi kadhaa za kiarabu za Magharibi mwa Asia.