Iran: Baraza la Usalama la UN lilaani shambulio la Marekani lililoua raia kwenye sherehe ya harusi
-
Gholamhossein Darzi
Iran imeliitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani shambulio la Marekani lililolenga nyumba ya makazi iliyokuwa ikiandaa sherehe ya harusi kusini mwa Jamhuri ya Kiislamu, ambalo limesababisha kuuawa shahidi wa raia watano, akiwemo mtoto wa miaka minne, na kuwajeruhi zaidi ya watu 70 wengine.
Gholamhossein Darzi, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu katika Umoja wa Mataifa, alitoa ombi hilo katika barua iliyoelekezwa kwa Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, na mwenyekiti wa Baraza la Usalama siku ya Jumatano, kufuatia wimbi jipya la mashambulio ya Marekani yanayolenga miji ya kusini mwa Iran, ambayo kwa ujumla yamesababisha vifo vya watu angalau 18 na kuwajeruhi wengine 108.
Akielezea mazingira ya shambulio hilo lililolenga sherehe ya harusi, mjumbe huyo alibainisha kuwa nyumba ya makazi katika Kouhestak, Wilaya ya Sirik, Mkoa wa Hormozgan, ililengwa wakati sherehe hiyo ikiendelea.
Amebaini kuwa: “Jamhuri ya Kiislamu inalaani vikali uhalifu huu wa kutisha na wa kikatili.” Aidha amesema: “kulenga kwa makusudi na kuua raia, wakiwemo watoto, ni ukiukaji mkubwa wa sheria za msingi za kibinadamu za kimataifa na ni sawa na uhalifu wa vita.”
Darzi amesema tukio la Kouhestak ni sehemu ya mfululizo wa mashambulio ya Marekani na Israel dhidi ya maeneo ya raia kote Iran.
Barua hiyo ilebainisha kuwa tangu Februari 28, mashambulio ya Marekani yamekuwa yakilenga raia na miundombinu muhimu mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na shule, hospitali, viwanja vya ndege, maeneo ya makazi, madaraja, barabara, na miundombinu ya reli.
Pia amekumbusha kuhusu shambulio la Februari 28 dhidi ya shule ya msingi katika mji wa Minab, Mkoa wa Hormozgan. Kwa mujibu wa barua hiyo, zaidi ya wanafunzi 168, wengi wao wakiwa wasichana wenye umri wa miaka saba hadi 12, pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule, waliuawa shahidi, huku wengine 110 wakipata majeraha.
Darzi amesema mashambulio ya kulipiza kisasi ya Iran mbele ya ukatili huo kama inayochukuliwa chini ya “haki yake ya asili ya kujihami chini ya Ibara ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.”
Amelitaka Baraza la Usalama kulaani ukatili huo, kushughulikia tukio la Kouhestak, kujumuisha mashambulio ya Minab na Kouhestak katika ripoti zijazo kuhusu ulinzi wa raia, kuwawajibisha Marekani kwa uharibifu uliosababishwa, na kudai fidia kamili.