Qalibaf: Iran na kambi ya Muqawama wako katika njia moja dhidi ya ubeberu
-
Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqir Qalibaf
Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa Iran na kambi ya Muqawama wako katika njia moja kukabiliana na ubeberu.
Mohammad Baqir Qalibaf amesema hayo katika mazungumzo yake na maafisa wa mawasiliano ya Kiislamu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kubainisha kwamba, hata serikali zinazoiunga mkono Marekani kwa dhati zinaiona Washington kuwa chanzo cha ukosefu wa usalama.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha katika mazungumzo yake na Bassem Naim, Mkuu wa Mawasiliano ya Kiislamu wa Harakati ya Hamas historia ya mapambano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kambi ya muqawama kuwa yenye mafunzo makubwa.
Qalibaf amesema: “Msingi na kiini cha mapambano haya ni vita kati ya haki na batili, pamoja na kukabiliana na ubeberu. Roho ya mapambano ya muqawama katika kipindi cha miaka 50 iliyopita imekuwa ikidhihirika kila mara kwa sura mpya.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akieleza kuwa asili ya kambi ya muqawama ni kupambana na dhulma, amesisitiza kuwa:
“Sisi hatukatai mazungumzo, lakini mazungumzo ni chombo cha mapambano. Na iwapo siku moja tutaacha kupambana na Marekani na utawala wa Kizayuni kwa njia mbalimbali, basi siku hiyo itakuwa siku ya kushindwa.
Akiashiria mazungumzo kati ya Iran na Marekani, amesema:
“Katika kifungu cha kwanza cha hati ya makubaliano, tulisisitiza kwamba vita vinavyoendeshwa na Marekani dhidi ya Iran na washirika wa Iran katika kambo ya muuqawama vinapaswa kumalizika. Hii ni licha ya kwamba upande wa pili, katika rasimu yake ya awali yenye vifungu 15, ulitaka kusitishwa kabisa shughuli za makombora, miradi ya nyuklia na muqawamai.”
Qalibaf, akieleza kuwa mihimili yote ya kambi ya muqawama iko katika umoja, amesema:
“Njia yetu inapaswa kuwa katika mwelekeo mmoja wa msingi, na tunapaswa kuhifadhi kambi ya muqawama ili uendelee na mapambano ya haki dhidi ya batili. Leo hii, hata serikali zinazoiunga mkono Marekani kwa dhati katika eneo hili zinakiri kwamba Marekani ndiyo inayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo.