Kuanzia shule ya Minab hadi harusi ya Kuhestak: Raia waendelea kuwa wahanga wa ukatili wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141168-kuanzia_shule_ya_minab_hadi_harusi_ya_kuhestak_raia_waendelea_kuwa_wahanga_wa_ukatili_wa_marekani
Jioni ya Jumanne, jeshi la Marekani lilishambulia kinyama sherehe ya harusi katika bandari ya Kuhestak, katika Wilaya ya Sirik kusini mwa Iran. Makumi ya watu waliuawa shahidi na kujeruhiwa; huku wanawake na watoto wakiwa miongoni mwa wahanga.
(last modified 2026-09-03T06:48:51+00:00 )
Sep 03, 2026 06:40 UTC
  • Kuanzia shule ya Minab hadi harusi ya Kuhestak: Raia waendelea kuwa wahanga wa ukatili wa Marekani

Jioni ya Jumanne, jeshi la Marekani lilishambulia kinyama sherehe ya harusi katika bandari ya Kuhestak, katika Wilaya ya Sirik kusini mwa Iran. Makumi ya watu waliuawa shahidi na kujeruhiwa; huku wanawake na watoto wakiwa miongoni mwa wahanga.

Mtoto wa miaka minne pia aliuawa shahidi. Sherehe hiyo ya harusi iligeuka kuwa eneo la jinai. Hili si shambulio la kijeshi tu; ni jinai dhidi ya raia. Watu wa Kuhestak hawakuwa katika uwanja wa vita; walikuwa wakifanya sherehe ya kawaida ya harusi, ambapo watoto pia waliungana na familia zao katika sherehe hiyo iliyopasa kuwa ya furaha. Lakini kinyume na matarajio, Marekani ilishambulia kikatili mkusanyiko huo wa raia, ambapo ilirusha kigaidi mabomu katikati ya familia zilizokuwa zikisherehekea harusi na kutokuwa na uhusiano wowote na uwanja wa vita. Kuhestak inawakilisha mwendelezo wa muundo wa mashambulio ya kinyama dhidi ya raia ambao awali ulionekana huko Minab na Lamerd. Katika siku ya kwanza kabisa ya vita shule ya msingi ilishambuliwa huko Minab, kisha ukumbi wa michezo ukashambuliwa katika mji wa Lamerd na sasa, sherehe ya harusi imelengwa huko Kuhestak.

Nukta ya pamoja inaonekana wazi katika mashambulizi hayo: Wahanga ni raia wa kawaidaa; watoto wanaopaswa kuwa shuleni, familia zinazopaswa kuwa pamoja, na watu wanaopaswa kusherehekea badala ya kupoteza maisha yao chini ya vifusi vinavyosababishwa na mabomu.

Katika kukabiliana na ukatili huo, Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Bunge la Iran, ameitaja Marekani kuwa "Shetani Mkuu." Leo, neno hili linabeba ujumbe muhimu zaidi kuliko ibara za kisiasa tu. Mwenendo wa Marekani katika uwanja wa vita umeweka wazi maana yake halisi. "Shetani Mkuu" ni nchi inayopigana vita maelfu ya kilomita kutoka mipaka yake yenyewe, huku ikijifanya kutoa mafunzo kwa dunia kuhusu haki za binadamu. Kwa miaka mingi, Washington imezigeuza haki za binadamu kuwa chombo cha kutoa mashinikizo ya kisiasa dhidi ya nchi nyingine, kuziwekea vikwazo serikali zisizotii amri zake, kutishia mataifa, na kutwisha wengine utamaduni wake usioendana na thamani zao za kimaadili. Lakini sasa Marekani hiyo hiyo inashambulia kikatili nyumba, shule, viwanja vya michezo, na sherehe za harusi nchini Iran bila kujali lolote.

Haki za binadamu hazipimwi kwa makombora na mabomu. Uaminifu wa kimaadili haujengwi kwa wingi wa kauli za kisiasa pekee. Serikali inayojionyesha kuwa mtetezi wa haki za binadamu lazima kwanza iwajibishwe kwa matendo yake yenyewe. Kuuawa shahidi watoto wa Iran kunapaswa kuchukuliwa kama kipimo cha madai ya Marekani kuhusu haki za binadamu, kipimo ambacho matokeo yake yanawekwa wazi mbele ya watu wote kuyaona. Ukatili wa Kuhestak pia umefichua kipengele kingine cha uhalisia wa vita. Hatari haipo tu katika shambulio lenyewe la mabomu, bali hatari kubwa zaidi ni kuona mashambulio ya kinyama kama hayo yakichukuliwa kuwa jambo la kawaida. Hatari ni kuona vifo vya watoto vikigeuzwa kuwa habari za kawaida, mauaji ya raia kupoteza uzito wake katika mtiririko mpana wa upashaji habari za vita, na dunia kuzoea kushuhudia ukatili wa aina hiyo.

Hata hivyo, uwajibikaji kuhusiana na suala hili haupaswi kuelekezwa kwa Marekani pekee; kimya cha Ulaya nacho ni sehemu ya mgogoro huu wa kimaadili. Serikali za Ulaya mara kwa mara hutoa taarifa kuhusu matukio ya kimataifa, kuzungumzia masuala ya haki za binadamu na eti kutetea sheria za kimataifa. Lakini, pale wanawake na watoto wa Iran wanapokuwa wahanga wa mashambulio ya Marekani, sauti zao za kulaani vitendo hivyo hazisikiki popote. Kimya hiki kina ujumbe wa kisiasa. Ulaya hutumia lugha tofauti linapokuja suala la mshirika wake Marekani. Ulaya hiyo hiyo, ambayo hudai kutetea haki za binadamu kama kanuni ya msingi katika masuala mengine, huamua kusalia kimya mbele ya mauaji ya kikatili ya raia wa Iran. Ni wazi kuwa undumakuwili huu kabla ya kudumisha uhalali wa haki za binadamu duniani, unafichua wazi sera za unafiki za nchi za Magharibi kuhusu suala hilo.

Taasisi za kimataifa nazo haziwezi kujificha milele nyuma ya pazia la ukimya. Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa ajili ya kutetea na kulinda maisha ya raia yanapokabiliwa na hatari. Baraza la Usalama lipo mahususi kwa ajili ya nyakati kama hizo. Mashirika ya haki za binadamu yaliundwa ili kuwatetea waathiriwa. Kusalia kimya mbele ya vifo vya watoto kunatilia shaka uhalali wa taasisi hizi. Kuhestak si mahali pa kijiografia tu; ni ushahidi wa kutekelezwa jinai dhidi ya binadamu. Inasimama kama ushahidi wa vita vilivyoanzishwa na Marekani, ambapo watu wa kawaida ndio wanaolipa gharama yake. Inashuhudia kisa cha mtoto ambaye hatarudi tena nyumbani kwao na familia ambayo sherehe yake ya harusi iligeuka kuwa msiba. Inasimama kama ushahidi wa dunia inayodai kutetea haki za binadamu lakini inakaa kimya mbele ya mauaji ya raia. Marekani inaweza kuficha ukatili huu ndani ya mafuriko ya habari za vita, Ulaya inaweza kuendelea kukaa kimya, na mashirika ya kimataifa yanaweza kutoa taarifa zisizo na msimamo thabiti kuhusu jinai hii, lakini ni wazi kuwa historia haikai kimya. Jinai ya Kuhestak haiwezi kufichwa na matamko ya kisiasa; itadumu katika kumbukumbu ya pamoja ya watu wa Iran na katika hukumu ya historia. Huko Kuhestak, Marekani kwa mara nyingine tena imefichua wazi sura halisi ya "Shetani Mkuu."