Jeshi la Iran lililenga ndege 370 za adui katika vita vya Marekani na Israel
-
Jeshi la Iran lililenga ndege 370 za adui katika vita vya Marekani na Israel
Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran kililenga zaidi ya ndege 370 za kivita za adui zikiwemo zenye rubani na zisizikuwa na rubani au droni wakati wa uchokozi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel.
Hayo yamesemwa na kamanda mwandamizi wa kijeshi, ambaye amebainisha sifa kwa mifumo iliyotengenezwa ndani ya nchi.
Brigadi Jenerali Mohammad Sadeghian, naibu mratibu wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran, amesema Ijumaa kuwa majeshi ya Iran yalitumia uzoefu wa vita vya siku 12 vya Juni mwaka jana kubaini udhaifu na kuimarisha ulinzi wao kabla ya vita kuanza tena Februari 28.
Amesema, “Kwa kutumia uzoefu wa thamani wa vita vya siku 12, kubainisha kwa usahihi nguvu zetu na kushughulikia udhaifu wetu, majeshi ya Iran yaliweza kujipanga kwa ajili ya vita vilivyoanza Februari 28 kwa namna ambayo zaidi ya ndege 370 za adui zililengwa."
Ameongeza kuwa “Ndege za kawaida za kivita zenye rubani na zisizokuwa na rubainiau droni za adui zilitunguliwa, jambo ambalo lilikuwa lisiloaminika kwa maadui.”
Sadeghian amesema kuwa droni ya kimkakati ya Marekani aina ya MQ-9 ilipigwa katika maji ya Ghuba ya Uajemi katika siku mbili zilizopita.
Taarifa hiyo inafuatia tangazo la Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwamba vikosi vyake vya ulinzi wa anga nchini vilitunua droni ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper katika Lango Bahari la Hormuz mapema wiki hii.
IRGC imesem droni hiyo ilipigwa na makuta ya makombora kutoka kwa vitengo vyake vya kisasa vya ulinzi wa anga kabla ya kuanguka katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Tukio hili la hivi karibuni linaongeza hasara zinazoripotiwa zilizopatikana na jeshi la droni za MQ-9 Reaper la Marekani tangu kuanza kwa uchokozi huo. Jeshi la Anga la Marekani limeitaja Reaper kama “zana muhimu zaidi” katika operesheni zake dhidi ya Iran.
Shirika la habari la Bloomberg hivi karibuni liliripoti kuwa Iran imetungua zaidi ya droni zisizozidi 24 za aina ya MQ-9 tangu kuanza kwa vita, ikiwakilisha takriban 20% ya idadi ya droni hizo iliyokuwepo kabla ya vita katika ghala la Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).
Kwa kuwa kile droni ya MQ-9 inagharimu takriban dola milioni 30, hasara hizo zinazoripotiwa zinakadiriwa kukaribian dola bilioni 1.