Admeri Sayyari: Uwezo wa Iran wa kuzuia mashambulizi umeongezeka pakubwa/ Taifa la Iran haliwezi kushindwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141250-admeri_sayyari_uwezo_wa_iran_wa_kuzuia_mashambulizi_umeongezeka_pakubwa_taifa_la_iran_haliwezi_kushindwa
Naibu Mkuu wa Jeshi la Iran amesema kuwa uwezo wa Jamhuri ya Kislamu wa kuzuia mashambulizi dhidi umeimarika pakubwa.
(last modified 2026-09-06T11:38:04+00:00 )
Sep 06, 2026 11:36 UTC
  • Admeri Habibollah Sayyari
    Admeri Habibollah Sayyari

Naibu Mkuu wa Jeshi la Iran amesema kuwa uwezo wa Jamhuri ya Kislamu wa kuzuia mashambulizi dhidi umeimarika pakubwa.

Admeri Habibollah Sayyari amesema hayo alipokuwa akizungumzia kauli za hivi karibuni za Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kuiwekea Iran mashinikizo, jambo linaloashiria kushindwa Washington kuchukua hatua katika medani ya vita.

Ameashiria uwezo wa kuzuia mashambulizi wa Jeshi imara la Iran baada ya vita vya siku 40 vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran, Admeri Habibollah Sayyari amesisitiza kuwa: "Wajibu wetu katika Jeshi ni kuimarisha uwezo wa kuzuia hujuma."

Ameongeza kuwa: Kutokana na uzoefu wenye tija tulioupata kutokana na vita vya siku 12 vilivyoanzishwa kwa pamoja na Marekani na Israel ikiwa ni pamoja na vita vya siku 40 (Vita vya Ramadhani) na Vita vya Hormuz; tumefanya juhudi kubwa kushughulikia udhaifu wowote na kuimarisha nguvu zetu kiasi kwamba uwezo wa nchi wa kuzuia mahambulizi na hujuma umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Katika kujibu kauli za Trump kuhusu mzingiro wa majini na wa kiuchumi dhidi ya Iran, Naibu Mkuu wa Jeshi la Iran amesema: Kuhusu kauli zisizo na msingi ambazo Trump amezitoa dhidi ya Iran tunaona kuwa anaendelea kurudia-rudia matamshi na kauli zisizo na msingi kama vile Wairani hawana silaha za nyuklia, tumeharibu majeshi yao ya majini na anga, hali yao ya kiuchumi ni mbaya na hawajalipwa mishahara yao."

Admeri Habibollah Sayyari amesema Trump hana kauli nyingine zaidi ya hizo, na tumezoea kauli hizi zisizo na msingi wala ukweli wowote."

"Maafisa wa Marekani wanajua vyema kwamba hawawezi kufanikisha lolote dhidi ya nguvu ya kivita, muqawama na azma ya wananchi adhimu wa Iran, amesisitiza Admeri Sayyari.