Baghaei: Uhusiano wa Iran na China ni mzuri sana, na mawasiliano yanaendelea katika ngazi mbalimbali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141274-baghaei_uhusiano_wa_iran_na_china_ni_mzuri_sana_na_mawasiliano_yanaendelea_katika_ngazi_mbalimbali
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran sambamba na kusisitiza kuendelea uhusiano mzuri na wa kirafiki kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China amesema, “Mawasiliano kati ya nchi hizo mbili yanaendelea kwa utaratibu na kwa mfululizo katika ngazi mbalimbali, na Iran itatumia fursa zilizopo mbele yake, zikiwemo Mkutano wa BRICS, kuendeleza mashauriano na China pamoja na nchi nyingine rafiki.”
(last modified 2026-09-08T08:32:07+00:00 )
Sep 07, 2026 11:00 UTC
  • Baghaei: Uhusiano w Iran na China ni mzuri sana, na mawasiliano yanaendelea katika ngazi mbalimbali
    Baghaei: Uhusiano w Iran na China ni mzuri sana, na mawasiliano yanaendelea katika ngazi mbalimbali

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran sambamba na kusisitiza kuendelea uhusiano mzuri na wa kirafiki kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China amesema, “Mawasiliano kati ya nchi hizo mbili yanaendelea kwa utaratibu na kwa mfululizo katika ngazi mbalimbali, na Iran itatumia fursa zilizopo mbele yake, zikiwemo Mkutano wa BRICS, kuendeleza mashauriano na China pamoja na nchi nyingine rafiki.”

Esmail Baghaei amesema hayo leo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari na kueleza kuwa, wiki iliyopita tulishuhudia matukio mengi, ndani ya nchi yetu na pia katika ngazi ya eneo. Tukio muhimu zaidi lilikuwa shambulio la kikatili na la kichokozi la Marekani dhidi ya Sirik, pamoja na kuuawa shahidi kundi la watoto na wananchi wa nchi hii, akiwemo mtoto shahidi Amir Ali Karimi katika sherehe ya harusi.

Aidha amesema, “Eneo letu liko katika hali ya misukosuko na mivutano mikubwa sana. Kwa upande mmoja, katika kipindi cha miezi sita iliyopita tumekabiliwa na uvamizi wa kijeshi unaoendelea wa Marekani dhidi ya nchi yetu. Uvamizi huo wa kijeshi ulianza tarehe 28 Februari, na kwa ushirikiano na utawala wa Kizayuni, umeendelea hadi leo kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuzingirwa kijeshi baharini na vita vya kiuchumi.

Akizungumzia kuendelea mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, “Uhalifu wa utawala wa Kizayuni Palestina na Lebanon unaendelea kwa ukali mkubwa. Mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi yanaendelea bila ya kukoma. Katika siku hizi chache zilizopita, tumeshuhudia kuendelea mauaji ya Wapalestina, wakiwemo watoto na wasichana wasio na hatia wa Palestina.