Kaimu Waziri wa Ulinzi: Iran inao uwezo kamili wa kuzishambulia manuwari za US zilizoweka mzingiro wa kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141314-kaimu_waziri_wa_ulinzi_iran_inao_uwezo_kamili_wa_kuzishambulia_manuwari_za_us_zilizoweka_mzingiro_wa_kiuchumi
Iran imeitoa maanani kikamilifu kauli iliyotolewa na Marekani ya kudogosha uwezo wake wa kijeshi na kusisitiza kwamba vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu vina teknolojia na utayari wa kuzilenga meli za kivita za Marekani zinazoshiriki katika mzingiro haramu wa majini uliowekwa dhidi ya taifa la Iran.
(last modified 2026-09-09T03:15:26+00:00 )
Sep 09, 2026 03:13 UTC
  • Kaimu Waziri wa Ulinzi: Iran inao uwezo kamili wa kuzishambulia manuwari za US zilizoweka mzingiro wa kiuchumi

Iran imeitoa maanani kikamilifu kauli iliyotolewa na Marekani ya kudogosha uwezo wake wa kijeshi na kusisitiza kwamba vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu vina teknolojia na utayari wa kuzilenga meli za kivita za Marekani zinazoshiriki katika mzingiro haramu wa majini uliowekwa dhidi ya taifa la Iran.

Katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB, Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Majid Ibn Reza, ametoa mjibizo kwa madai ya maafisa wa Marekani kwamba Iran haina uwezo wa kushambulia meli zinazotekeleza mzingiro wa kiuchumi, baada ya mwandishi wa habari wa IRIB kusema: "Wamarekani wanaamini kuwa hatuna uwezo na teknolojia ya kulenga manowari zinazoshiriki katika mzingiro wa kiuchumi dhidi ya watu wetu".

Katika mjibizo wake kwa kauli hiyo, Brigedia Jenerali Majid Ibn Reza alisema: "Inshaa Alllah utaona; utayaona matokeo."

Aliposhikiliwa aeleze bayana kama Wamarekani wawe na uhakika juu ya uwezo wa Iran, Jenerali Ibn Reza alirudia kusema: "Inshaa Allah, bila shaka yoyote mtayaona matokeo".

Matamshi hayo yametolewa wakati Washington inaendeleza mzingiro wake wa baharini kinyume cha sheria dhidi ya bandari za Iran, ambao ni kitendo cha uchokozi wa kiuchumi unaoelezewa kila mara na maafisa wa Iran kuwa ni mwendelezo wa vita vya kichokozi vilivyoanzishwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu mapema mwaka huu.

Mamlaka za Iran zimekuwa zikisisitiza kwamba hatua kama hizo ni ukiukaji wa mamlaka ya uhuru wa nchi na sheria za kimataifa, na kwamba watu wa Iran na vikosi vyao vya ulinzi hawatasalimu amri kwa mashinikizo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina sekta yake yenyewe ya ulinzi inayotegemea uwezo wake wa ndani, ambayo imejengwa na kuendelezwa katika mazingira ya vikwazo vikali kabisa. Imeweza kutengeneza makombora ya kisasa ya kushambulia meli, na kuunda ndege zisizo na rubani, na mifumo mingine yenye uwezo wa kuzifanya mali za maadui wa baharini ziwe hatarini katika Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman, na kwingineko…/