Ripoti: Hatua kali za kulipiza kisasi za Iran zachagiza mipango ya Marekani ya kujiondoa Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141328-ripoti_hatua_kali_za_kulipiza_kisasi_za_iran_zachagiza_mipango_ya_marekani_ya_kujiondoa_asia_magharibi
Maafisa wa jeshi na ujasusi wa Marekani wanajadili kimya kimya kupunguza pakubwa uwepo kijeshi wa Washington katika eneo la Asia Magharibi baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran kusababisha vifo vingi na kuharibu kambi na vituo vya ujasusi vya Marekani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya jana Jumanne ya CNN.
(last modified 2026-09-09T11:10:28+00:00 )
Sep 09, 2026 11:07 UTC
  • Ulipizaji kisasi wa Iran wachagiza mipango ya Marekani kuondoka Asia Magharibi
    Ulipizaji kisasi wa Iran wachagiza mipango ya Marekani kuondoka Asia Magharibi

Maafisa wa jeshi na ujasusi wa Marekani wanajadili kimya kimya kupunguza pakubwa uwepo kijeshi wa Washington katika eneo la Asia Magharibi baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran kusababisha vifo vingi na kuharibu kambi na vituo vya ujasusi vya Marekani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya jana Jumanne ya CNN.

Majadiliano hayo yanalenga kuandaa kile ambacho maafisa wamekielekeza kama "mkakati mwingine wa baada ya tukio la Septemba 11," kufuatia vita hivyo kufichua "udhaifu mkubwa" katika miundo mbinu ya kijeshi ya Washington katika eneo la Asia Magharibi.

Ripoti ya CNN imebainisha kuwa maafisa wa Marekani "sasa wanachukua hatua kwa uchache kutabiri nini kinaweza kukubalika" kwa Rais Donald Trump, ambaye wamemtaja kama "rais ambaye hubadilisha ghafla misimamo yake " na ambaye hadi sasa "hajaweka wazi mkakati wowote wa wakati ujao baada ya vita."

Marekani ina takriban wanajeshi 50,000 waliotumwa katika maeneo mbalimbali Asia Magharibi, wakiwa na mtandao mkubwa wa kijeshi ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na makombora pamoja na ndege zisizo na rubani za Iran tangu kuanza vita.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa mashambulio ya Iran yamewajeruhi maelfu ya wanajeshi wa Marekani na kuua wengine 18, huku kituo cha Jeshi la Wanamaji la Marekani la Kikosi cha Tano (Fifth Fleet) nchini Bahrain na vituo vingine vya Marekani vikipata hasara na uharibifu mkubwa.

"Maafisa wa shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) waliorudishwa nyumbani wakati mapigano yaliposhtadi mapema mwaka huu wanarejeshwa katika Asia Magharibi", imeeleza duru moja ya habari katika mahojiano na televisheni ya CNN.

Vikosi vya Marekani sasa vinafanya tathmini juu ya namna ya kuimarisha zaidi ngome zao zilizosalia, ikiwa ni pamoja na kuhamishia baadhi ya kambi chini ya ardhi ili kuwalinda wanajeshi wake dhidi ya mashambulizi zaidi ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Iran.