Msemaji wa Jeshi la SEPAH: Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141340-msemaji_wa_jeshi_la_sepah_marekani_haina_uwezo_tena_wa_kuendelea_kuwepo_asia_magharibi
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo katika eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2026-09-10T03:24:01+00:00 )
Sep 10, 2026 03:22 UTC
  • Msemaji wa Jeshi la SEPAH: Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo Asia Magharibi

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo katika eneo la Asia Magharibi.

Brigedia Jenerali Hussein Mohebi amesema hayo katika mahojiano yake na Shirika la Habari la Iran (IRNA) na kubainisha kwamba, “Mlango-Bahari wa Hormuz leo ni miongoni mwa mambo muhimu yanayoamua mfumo wa utaratibu wa dunia na hatima ya vita. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kutumia uwezo wake wa kijiografia, kiutendaji na kijeshi, ina udhibiti na mamlaka madhubuti juu ya eneo hili.”

Amesema, “Mlango-Bahari wa Hormuz si njia ya baharini tu, bali umegeuka kuwa miongoni mwa mambo muhimu yanayoamua mfumo wa utaratibu wa dunia na matukio  ya vita. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikiwa na uwezo wa kijeshi, kiutendaji na wa silaha, inatumia uwezo wake katika kusimamia na kudhibiti eneo hili la kimkakati.

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), akizungumzia kupungua kwa uwepo wa meli za kivita za Marekani katika Ghuba ya Uajemi, amesema:

‘Kabla ya kuanza mapigano ya hivi karibuni, kulikuwa na takribani meli 30 hadi 40 za kivita za Marekani katika eneo hili. Lakini leo hali hiyo haionekani tena, na sehemu kubwa ya meli za kivita za nchi hiyo zimejiondoa na kuwa umbali wa mamia ya kilomita kutoka pwani ya Iran.’”

Brigedia Jenerali Mohebi ameongeza kusema kuwa, “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kutumia silaha na makombora mapya, ina uwezo wa kulenga na kuharibu vifaa vya adui vilivyo katika umbali mrefu. Uwezo huu umeongeza gharama za kuendelea kuwepo na kufanya operesheni kwa vikosi vya Marekani katika eneo hili.

Kadhalika amesema kuwa, Marekani inakabiliwa na udhoofu mkubwa wa nguvu kazi na vifaa katika eneo hili. Ameendelea kusema kwamba, udhoofu huo hauishii kwenye vifaa na meli za kivita pekee, bali pia umeathiri hali ya kisaikolojia na kiakili ya wanajeshi walioko katika eneo hili. Kuendelea hali hii kunazidi kuisababishia Marekani gharama kubwa.