Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Tukio la Ashuraa ni somo la kivitendo la jinsi ya kuishi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i48294
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa tukio la Ashuraa mwaka 61 Hijria katika ardhi ya Karbala ni somo la kivitendo la jinsi ya kuishi na kuongeza kuwa, Imam Hussein bin Ali (as) ni kigezo cha kuigwa na mataifa yote hususan mataifa ya Iran, Iraq, Syria, Yemen na Bahrain na amewafundisha wanadamu wote huru duniani jinsi ya kusimama kidete na kuwa na ari na ghera ya kulinda matukufu na thamani za kibinadamu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 21, 2018 13:57 UTC
  • Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Tukio la Ashuraa ni somo la kivitendo la jinsi ya kuishi

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa tukio la Ashuraa mwaka 61 Hijria katika ardhi ya Karbala ni somo la kivitendo la jinsi ya kuishi na kuongeza kuwa, Imam Hussein bin Ali (as) ni kigezo cha kuigwa na mataifa yote hususan mataifa ya Iran, Iraq, Syria, Yemen na Bahrain na amewafundisha wanadamu wote huru duniani jinsi ya kusimama kidete na kuwa na ari na ghera ya kulinda matukufu na thamani za kibinadamu.

Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Hassan Abu Turabifard amesema kuwa mantiki ya harakati ya mpambano ya siku ya Ashuraa ilitekelezwa katika kipindi cha kujitetea kutakatifu hapa nchini Iran. Ameongeza kuwa, kipindi cha kujitetea kutakatifu kilikuwa somo na darsa la kusimama imara kwa watu wa Lebanon na Iraq na kiliwafundisha jinsi ya kupambana na uistikbari na mabeberu.

Abu Turabifard ameashiria falsafa ya mienendo ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu na Mwanamfalme  wa Saudi Arabia Muhammad bin Salman dhidi ya taifa la Iran na kusema: Tajiriba ya miongo mine iliyopita ya taifa la Iran iko mbele ya Marekani na jamii ya kimataifa, na taifa la Iran litaendela kushikamana na harakati ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Hussein (as) katika njia ya kuelekea kwenye ushindi.

Wakazi wa jiji la Tehran katika Sala ya Ijumaa 

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia ameashiria wasiwasi wa Waziri Mkuu wa Israel kuhusu kambi ya muqawama na mapambano katika eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa, Israel inajua vyema kwamba, wakati wa kuangamia kwake umewadia.

Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as) aliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria katika harakati kubwa ya mapambano na mageuzi dhidi ya utawala dhalimu wa Banii Umayyah.