Marasimu ya Kimataifa ya "Watoto Wanaonyonya wa Hussein" yafanyika katika nchi zaidi ya 40
Marasimu ya Kimataifa kwa jina la "Watoto Wachanga Wanaonyonya wa Hussein a.s" yamefanyika leo Ijumaa katika zaidi ya maeneo elfu sita katika Iran ya Kiislamu na katika nchi 45 duniani sambamba na Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram.
Marasimu hayo ya Kimataifa ya Watoto Wachanga wanaonyonya wa Hussein a.s ni mjumuiko wa kidini unaofanywa na Waislamu duniani ikiwemo hapa Iran, India, Pakistan, Iraq, Saudia, Uturuki na Afghanistan katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram katika kuwakumbuka watoto waliouliwa shahidi katika Siku ya Ashura.
Katika marasimu haya, akina mama huwavalisha watoto wao wanaonyonya maziwa mavazi yenye kufanana na kisha huwafunga vipande vya vitambaa kichwani vilivyoandikwa jina tukufu la Ali Asghar a.s.; na hivyo kudhihirisha mapenzi na kujitolea kwao kwa familia hiyo tukufu na adilifu.

Mtukufu Ali Asghari a.s alikuwa mtoto mdogo zaidi wa Imam Hussein a.s; Imamu wa tatu wa Waislamu wa Kishia ambaye aliuliwa shahidi tarehe Sita Muharram mwaka 61 Hijria huko Karbala akiwa na umri wa miezi sita.