May 31, 2023 11:24 UTC
  • Nasser Kan'ani
    Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba: "Nyumba ya buibui haiwezi kutegemewa na jitihada za kupanua uwepo wa utawala haramu wa Israel kikanda hazitasaidia kukarabati msingi inayoyumba ya utawala bandia wa Kizayuni."

Nasser Kan'ani amesema katika ujumbe  huo wa Twitter kwamba: Hakuna harakati yoyote ya kikanda itakayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel bila ya kutambuliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameendelea kuandika kwamba: Utawala wa Kizayuni wa Israel unachukiwa na mataifa ya dunia na hautakuwa na mustakabali mwema.

Inaonekana kwamba ujumbe huo wa Twitter ni jibu kwa ziara ya rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Jamhuri ya Azerbaijan.

Rais wa Israel, Isaac Herzog, aliwasili Baku, mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, jana (Jumanne, Mei 30).

Licha ya upinzani wa jumii ya Wislamu wa madhehebu ya Shia na ya kidini ya nchi hiyo, serikali ya Jamhuri ya Azerbaijan ilifungua ubalozi wake mjini Tel Aviv mwanzoni mwa mwaka huu, ikiendelea kustawisha uhusiano wake na utawala wa Kizayuni unaoendelea kuua raia wasio na hatia wa Palestina na kukalia kwa mabavu kibla cha kwanza cha Waislamu.

Tags