Dec 08, 2023 15:10 UTC
  • Maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen kuiunga mkono Palestina

Wananchi wa Yemen leo asubuhi wamefanya maandamano kadhaa na kusisitiza udharura wa kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina mkabala wa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakazi wa mkoa wa Saada huko Yemen mapema leo Ijumaa walifanya maandamano manne makubwa chini ya anwani "Tunaendelea kuiunga mkono Gaza na tupo tayari kwa machaguo yote." Maandamano hayo yamefanyika katika makao makuu ya mkoa wa Sa'ada, na katika mikoa mengine ya Yemen.

Wananchi wa Yemen walioshiriki katika maandamano lhayo walikuwa wamebeba bendera za Yemen na Palestina huku wakipiga nara kama "raia wa Gaza hamko pekee yenu", "wananchi wenye imani wako pamoja nanyi" n.k. 

Katika maandamano hayo ya leo, wananchi wa Yemen walisoma mashairi ya hamasa ya kuunga mkono mapambano na istiqama ya kishujaa ya wananchi wa Palestina.  Wananchi wa Yemen pia wamelaani misimamo ya watawala madhalimu ya kuunga mkono mashambulizi ya kikatili dhidi ya Gaza na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wakazi wa ukanda huo.

Mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni, Gaza 

Washiriki katika maandamano ya leo huko Yemen wametaka kuonyeshwa ipasavyo taswira ya jinai zinazofanywa kila uchao na utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza ili kuwafunua macho walimwengu kuhusu jinai hizo dhidi ya Waislamu. Hadi sasa jeshi la Yemen limefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya ngome za Wazayuni kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni), makombora na kusimamisha meli za Wazayuni katika Bahari Nyekundu. 

Tags